Wapiganaji wa Rapid Support Forces wametekeleza uhalifu dhidi ya binadamu wakati wakizuia watu kuondoka El-Fasher jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulisema siku ya Ijumaa.
Wanaotekeleza zaidi uovu huu ni RSF katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinaingia mwaka wake wa tatu sasa, ujumbe huo ulisema kwenye ripoti yake ambayo ilisisitiza uchunguzi uliofanyika hapo awali.
"RSF pia imefanya uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mauaji ya watu wengi, dhulma za kingono, uporaji, na uharibifu wa maisha ya watu— wakati mwingine ikiwa ni pamoja na mateso na uangamizaji wa watu," mwenyekiti wa ujumbe, Mohamed Chande Othman, alisema katika taarifa.
Kuzuia watu kutoka
Kamati hiyo ya watu watatu ya Umoja wa Mataifa imepewa majukumu na Baraza la Haki la Binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza ukiukwaji huo wa haki.
Inasema kuwa ripoti yake ya hivi karibuni inatokana na mahojiano ya zaidi ya 200, nyingi yakiwa na walionusurika machafuko, pamoja na video na ripoti zilizowasilishwa na mashirika ya kiraia.
Maelfu ya watu wamekuwa wakizuia kutoka katika eneo ambalo ni ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan huko El-Fasher, makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini, ambapo sasa ndiyo kuna mapigano.
Ripoti hiyo ya kurasa 18, 'Vita vya Kikatili', inasema RSF na washirika wake wametumia kuweka watu wakia na njaa kama mbinu ya vita, kuwanyima raia misaada kama chakula na dawa.
Vita hivyo vilianza Aprili 2023 wakati jeshi na RSF walipotofauatiana kuhusu mipango ya kuwajumuisha wapiganaji wake kwenye jeshi.