AFRIKA
1 dk kusoma
Watoto 200 wafariki katika maporomoko ya ardhi Sudan - shirika la misaada
Shirika la Save the Children linasema watu 150, ikiwemo watoto 40, wamenusurika na wanatibiwa kwa sasa.
Watoto 200 wafariki katika maporomoko ya ardhi Sudan - shirika la misaada
Miili 300 imepatikana katika kijiji cha Tarseen, nchini Sudan baada ya maporomoko ya ardhi. / Reuters
tokea masaa 12

Mapromoko hatari ya ardhi katika eneo la magharibi mwa Sudan la Darfur mwishoni mwa wiki limesababisha vifo vya watoto wasiopungua 200, shirika la misaada lilisema Ijumaa, huku juhudi za uokoaji zikiendelea katika eneo hilo.

Watu zaidi 1,000, wengi wao wamefukiwa kwenye matope, wanaaminika kupoteza maisha yao katika maporomoko ya Agosti 31.

Save the Children linasema watu 150, ikiwemo watoto 40, wamenusurika na wanatibiwa kwa sasa.

“Hili ni janga juu ya janga ambalo kwa sasa ni mgogoro nchini Sudan. Haya ni moja ya majanga mabaya zaidi kuwahi kutokea Sudan,” Mkurugenzi wa operesheni wa Save the Children nchini Sudan, Francesco Lanino, ameliambia shirika la AP siku ya Ijumaa.

Sudan tayari ilikuwa inakumbwa na hali mbaya zaidi kwa watu duniani iliyosababishwa na vita vya wenyewe tangu vilipoanza Aprili 2023 katika mji mkuu, Khartoum.

Mamlaka nchini Sudan zilipata miili ya watu 375 siku ya Alhamisi waliofariki katika maporomoko ya ardhi kufuatia mvua kubwa ilionyesha kwa siku kadhaa katika kijiji cha Tarasin kwenye Milima ya Marrah.

Shirika la Save the Children na mashirika mengine ya misaada yanapeleka misaada kwa watu walioathirika na kuwasaidia kuwasafirisha hadi katika maeneo salama kwa kutumia ngamia na punda.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us