AFRIKA
3 DK KUSOMA
Kumbukumbu ya shujaa wa uhuru wa DRC Lumumba
Tarehe 30 Juni ni kumbukumbu ya uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Kumbukumbu ya shujaa wa uhuru wa DRC Lumumba
Remembering DRC's independence hero LumumbaJune 30 is Democratic Republic of Congo's independence anniversary. / Photo: AP
2 Julai 2023

Patrice Lumumba alikuwa kiongozi shupavu katika harakati za uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zilizopigana dhidi ya wakoloni wa Ubelgiji. Alikua Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi mnamo Juni 1960.

Hata hivyo, aliuawa takriban miezi sita baada ya kupata nafasi ya uongozi. Alikuwa na umri wa miaka 35. Kuna mambo machache ya kuvutia kuhusu maisha ya Patrice Lumumba.

Jino la Lumumba

Jino la taji la dhahabu la Patrice Lumumba tangu wakati huo limekuwa alama ya kihistoria. Jino hilo ndilo pekee lililobaki kwake baada ya mwili wake kuripotiwa kuyeyushwa kwa kumwagiwa tindikali maarufu kama asidi.

Jino hili lilikaa Ubelgiji kwa miongo kadhaa kabla ya hatimaye kurejeshwa kwa familia yake huko DRC mnamo Juni 2022 kufuatia uamuzi wa mahakama ulioamuru kurejeshwa.

Baada ya kutua Kinshasa, jino hilo lilizunguka sehemu kadhaa za DRC likiwa kwenye jeneza. Jino hilo lilizikwa mnamo Juni 27 2022 kwa mazishi ya heshima na itikadi za serikali.

Kubadilisha jina

Alizaliwa Élias Okit'Asombo lakini akabadilisha jina lake kuwa Patrice Lumumba. Wanahistoria wanasema wakazi wa kizungu nchini Kongo walipata shida kutamka jina lake la Kiafrika.

Kuna chama cha kisiasa kinachojulikana kama Unified Lumumbist Party, ambacho kilianzishwa na mwanae, François ambaye pia sasa ni mwanasiasa nchini DRC.

Heshima ya kitaifa

Patrice Lumumba anakumbukwa hasa Juni 30, wakati DRC inaadhimisha uhuru wake.

Kuna sanamu ya kifahari ya Lumumba katika mji mkuu Kinshasa. Kuna sanamu zingine za mwana-Africanist mahali pengine kote nchini. Kaburi lake pia lipo kwa lengo la kuhifadhi urithi wake.

Ubelgiji na Marekani zilishutumiwa kwa kuhusika katika mauaji ya Patrice Lumumba.

Mnamo 2002, Ubelgiji iliomba radhi kwa kuhusika na kifo chake.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us