AFRIKA
2 DK KUSOMA
Sekta ya elimu Kenya kufanyiwa mabadiliko mara moja
Rais William Ruto amesema mabadiliko haya yanalenga kuboresha ubunifu na kurahisisha wanafunzi kuibua vipaji vyao
Sekta ya elimu Kenya kufanyiwa mabadiliko mara moja
Kenya yafanya mabadiliko katika mfumo wake wa elimu  / picha: Reuters
2 Agosti 2023

Rais William Ruto amesema mfumo wa elimu nchini utafanyiwa mabadiliko mara moja.

Hii inafuatia uzinduzi wa ripoti ya utafiti katika sekta ya elimu, jumanne, iliyotoa mapendekezo tofauti ya kuboresha sekta ya elimu.

"Elimu ni msingi wa maendeleo ya mtaji wetu, " Rais William Ruto alisema akipokea ripoti hiyo, " ndiyo maana serikali inawekeza kwa makusudi katika elimu bora,"

Je , mabadiliko gani yamewekwa katika elimu?

  • Maeneo ya mafunzo yatapunguzwa ili kuwapunguzia wanafunzi mrundiko wa kazi nyingi shuleni

  • Mafunzo ya mazingira na hatua za mabadiliko ya tabianchi kufanywa katika taasisi zote za mafunzo

  • Kutakuwa na miezi mitatu ya huduma kwa jamii kwa wahitimu wa shule ya sekondari kabla ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu

  • Baadaye watafanya miezi 9 zaidi ya huduma ya lazima ya jamii baada ya kumaliza elimu ya juu. Watapewa cheti cha kumaliza huduma ya jamii kama uthibitisho kabla ya kuingia katika soko la ajira

  • Kenya inaanzisha operesheni ya chuo kikuu kipya kinachoitwa Open University of Kenya ambacho kitatoa masomo kupitia mitandaoni. Wanafunzi wa kwanza watatarajiwa kuingia katika chuo mwezi Septemba 2023. Hii inatarajiwa kufanya gharama ya elimu kwa chuo kikuu iwe ya bei nafuu zaidi na kuwa rahisi kupatikana

  • Taasisi za mafunzo ya kiufundi zitaunganishwa na viwanda husika

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us