Na Dayo Yussuf
Garissa Kaskazini Mashariki mwa Kenya ni mojawapo ya maeneo yenye joto jingi nchini huku halijoto wakati mwingine ikipanda hadi nyuzi joto 40 Celcius. Mandhari ni mchanganyiko tambarare na milima.
Lakini ina utajiri mkubwa, hasa iwapo kama vile wenyeji, unazingatia utajiri kuwa mifugo.
Madereva mara nyingi wanalazimika kuwapisha maelfu ya Ngamia, ng'ombe na mbuzi wanaovuka barabara kwa muongozo wa wachungaji wao.
Takriban kilomita 10 kutoka barabara kuu utakutana na kambi ya Hagadera. Kambi ya pili kwa ukubwa ya wakimbizi duniani. Inawahifadhi zaidi ya watu 100,000 na bado wanaendelea kuja kila uchao.
Lakini pengine barabara kama hii hungetarajia kukutanana Batula Ali Abdullah.
Anafanya kazi kama dereva wa gari la wagonjwa la ambulensi kati ya Kambi ya Hagadera na Hospitali kuu ya Garissa ambapo hutoa uhamishaji wa dharura unaohitajika kwa wagonjwa walio katika hatari kubwa.
‘’Nimekuwa dereva kwa takriban miaka 15. Nilifanya kazi ya udereva katika wizara ya kazi lakini tangu 2019 nilianza kufanya kazi ya udereva wa gari la wagonjwa.’’ Batula anaambia TRT Africa.
Mara alipohitajika Batula alijikuta anachukua zamu ya dereva wa ambulensi na tangu hapo hakurudi nyuma tena.
‘’Nimepata wito wangu hapa.’’ Anasema. ‘’ Naona furaha sana ninapowafikishia watu msaada wa dharura. Nimewabeba wanawake waliokuwa kwenye hatari ya kufa kwa kuvuja damu kupita kiasi. Niliwakimbiza hospitalini wakaokolewa.’’ Anaongeza.
Batula hakuwahi kujiona katika taaluma ya matibabu. Lakini katika miaka minne iliyopita, ameshuhudia binafsi kuwa katika hali ngumu. Anasema ameona jinsi mchango wake mdogo unavyoweza kusaidia watu wenye uhitaji mkubwa wa msaada wa matibabu.
‘’Nimewasaidia baadhi ya wanawake kujifungua na kusaidia kukata kitovu. Ilinifanya nihisi kukimbilia. Nilihisi msaada sana,’’ anasimulia kwa hisia ya kuridhika.
Wanawake wanahisi furaha
Batula sasa ana nia ya kuimarisha ujuzi wake wa matibabu kwa mafunzo zaidi. ‘’Nafikiria kwenda kupata mafunzo sasa kama nesi au mkunga. Nadhani kuna kitu maalum katika kusaidia kuleta mtu katika ulimwengu huu. Inaridhisha sana,’’ anaongeza.
Hadithi ya Batula imekuwa ikizunguka Kenya na baadhi ya maeneo ya nchi jirani ya Somalia. Anasema wanawake wengi hufurahi na wanapata utulivu zaidi anapokuwa kwenye kiti cha udereva.
‘’Wanawake wenye asili ya Kisomali kwa kawaida huwa na haya wanapohudumiwa na wanaume. Ninapokuwa huko na ninaweza kuwasaidia, wanafurahi sana. Wakati mwingine wananiomba nije kuwasaidia,’’ anaiambia TRT Afrika.
Wengine wanasema hii inaangazia hitaji la wanawake zaidi katika taaluma ya matibabu na huduma za dharura. ‘’Natamani kuona wanawake na wasichana wengi zaidi katika taaluma hii. Wanaweza kufanya hivyo,’’ anasema.
Kukabiliana na changamoto
Batula inawatia moyo wasichana wadogo kutoka eneo hilo na kuongeza matumaini ya kuongeza idadi ya madereva wa ambulensi ya kike na madaktari.
‘’Wasichana wadogo wanaponiona ‘nikiruka kwa kasi sana’ katika gari la wagonjwa, huku ving’ora vimewashwa, wanashangilia. Wananiuliza kama wanaweza pia kuwa madereva wa ambulensi kama mimi,’’ anasema.
Safari ya kukubalika kama dereva wa gari la wagonjwa haikuwa rahisi kila wakati.
Batula anasema mwanzoni, alikumbana na upinzani kutoka kwa baadhi ya wanafamilia wake na jamii ambao walihisi anavunja utamaduni.
‘’Mwanzoni hawakuelewa. Lakini sasa wanafurahi sana nami. Wanajivunia kazi yangu.’’
Kazi ya udereva wa gari la wagonjwa hudai kujitolea kamili na inachukua muda wakati mwingine na simu za saa isiyo ya kawaida kulingana na dharura. Batula anasema hii ni moja ya changamoto.
Hata hivyo, anasema, hii inamtia moyo badala ya kuwa kikwazo. Anaamini mbali na kuridhika kwa kazi anayopata, watu wengi wanamtegemea kwa matunzo na ushawishi.