AFRIKA
2 DK KUSOMA
Zimbabwe yafanya uchaguzi mkuu
Takriban watu milioni sita na laki sita walijisajili kupiga kura katika taifa hilo lenye idadi  ya takriban watu milioni 15
Zimbabwe yafanya uchaguzi mkuu
Wananchi Zimbabwe wanapiga kura kuchagua rais na viongozi wengine / picha : AFP 
23 Agosti 2023

Takriban watu milioni sita na laki sita walijiandikisha kupiga kura katika taifa hilo lenye idadi ya takriban watu milioni 15.

Akipiga kura yake katika mji alikozaliwa wa Kwekwe, katikati mwa Zimbabwe, rais wa sasa Emmerson Mnangagwa anayegomea kiti kwa awamu ya pili, aliwaambia waandishi wa habari,

"Kama nadhani sitachukua, basi nitakuwa mjinga."

Nelson Chamisa mgombea mwingine anaonekana kama mpinzani mkuu wa rais Mnangangwa.

Matokeo ya ubunge yanatarajiwa kuanza kutangazwa kufikia Alhamisi asubuhi. Matokeo ya urais yanatarajiwa kuja baadaye, ingawa ni ndani ya siku tano.

Ili kushinda urais, mgombea lazima apate zaidi ya 50% ya kura.

Ikiwa hakuna mshindi wa moja kwa moja, marudio ya uchaguzi yatafanywa kati ya wagombea wawili wa juu yatafanyika Oktoba tarehe 2.

Wagombea wa kura za udiwani wanahitaji puta wingi wa kura zilizopigwa ili kutangazwa washindi

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us