D-Voice: Kinda wa kundi la muziki Tanzania, Wasafi, azidi kutamba
D-Voice: Kinda wa kundi la muziki Tanzania, Wasafi, azidi kutamba
Chini ya mwezi tu tangu azinduliwe na Wasafi, Dvoice, amezidi kutawala 'chati' huku akizidi kujizolea sifa na kuthibitisha kwa nini Diamond Platnumz amemsajili kwenye lebo ya Wasafi
30 Novemba 2023

Mwimbaji mchanga D-Voice, majina kamili Abdul Khamis Ali Mtambo, anazidi kutamba na nyimbo zake siku chache tu tangu uzinduzi wake na lebo tajika ya mziki Tanzania, Wasafi.

Mchipukizi huyo wa Wasafi, lebo inayomilikiwa na mwanamuziki maarufu Afrika, Diamond Platnumz, aliyezaliwa Rufiji, amefikisha zaidi ya wafuasi 100,000 kwenye ukurasa wake wa YouTube huku wimbo wake wa BamBam aliomshirikisha Zuchu, ukitazamwa na zaidi ya watu milioni moja.

Aidha, wimbo huo wa D-Voice na Zuchu, pia ndio umechaguliwa kuwa wimbo wa wiki kupitia kampuni ya upakuaji wa muziki Afrika - Boomplay.

Mtoto wa tatu kwenye familia aliyezaliwa 2004, hajatudi nyuma tangu kuzinduliwa rasmi mnamo tarehe 16 Novemba.

Tangu ajiunge na Wasafi, ameachilia nyimbo 10 zikiwemo Umenifunza, Mtamu, BamBam, Mpeni Taarifa, Chori Chori, Nimezama, Turudiane, Kama Wengine, Mungu Baba na lolo ambazo baadhi, amewashirikisha wasanii wa Wasafi akiwemo Diamond Platnumz, Lava Lava, Zuchu, na Mbosso.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us