AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania: Jakaya Kikwete ‘awashangaa’ waliopinga uteuzi wa Samia Suluhu Hassan
Rais huyo mstaafu wa Tanzania, amekosoa hatua ya baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupinga uamuzi wa chama hicho kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa chama hicho.
Tanzania: Jakaya Kikwete ‘awashangaa’ waliopinga uteuzi wa Samia Suluhu Hassan
Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete./Picha:Wengine
tokea masaa 12

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameoneshwa kushangazwa na baadhi ya watu waliotaka Rais Samia Suluhu Hassan asigombee urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akihoji kwanini hawakufanya hivyo kwa wakuu wa nchi wa serikali za awamu zilizopita.

Akizungumza Agosti 29, 2025, wakati wa uzinduzi wa kampeni za nchi nzima za chama hicho, zilizofanyika katika viwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam, Kikwete alidai kuwa wale wanaofanya hivyo, wanafanya kwa makusudi au wanajitoa ufahamu.

“Na mimi nililaumiwa kwa maneno niliyoyasema, na sasa nasema wanaotasema hayo ama wanajisahaulisha au wanajitoa ufahamu. Utaratibu wanaujua na walikuwepo,” alisema kiongozi huyo mstaafu.

Kauli ya Kikwete inakuja huku kukiwepo madai ya malalamiko kutoka baadhi ya wanachama wa chama hicho, akiwemo aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, aliyedai kupitia mitandao ya kijamii kuwa, utaratibu uliotumika kumpitisha Rais Samia, ulikiuka taratibu za chama hicho.

“Mbona haya hatujayasikia kwa hayati Benjamin Mkapa, Kikwete wala Magufuli?Kinachonishangaza, hao wanaojifanya kimbelembele kuyasema haya wao nao walikuwepo,” alisema Kikwete.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us