UTURUKI
3 dk kusoma
Uturuki yalaani mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza yataka Jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua
Naibu Mwenyekiti wa Haki za Binadamu wa Chama cha Haki na Maendeleo (AK) cha Uturuki, Hasan Basri Yalcin, amelaani vikali mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel dhidi ya Gaza.
Uturuki yalaani mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza yataka Jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua
Ujumbe wa Uturuki wa Chama cha AK katika Mpaka wa Rafah unaangazia mshikamano na watu wa Gaza huku kukiwa na mzozo unaoongezeka. /
8 Septemba 2025

Yalcin ametoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja, kushtakiwa wahusika na kesi za uhalifu wa kivita, na kufanikisha suluhisho la mataifa mawili.

Chama tawala cha Uturuki AK , kimekosoa kampeni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza kwa kuzitaja kama mauaji ya halaiki, huku Naibu Mwenyekiti wake wa Haki za Binadamu, Hasan Basri Yalcin, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na kuahidi mshikamano wa Ankara na Wapalestina.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika Kituo cha Mpaka cha Rafah Jumatatu, Yalcin alisema Israel inaendesha ukandamizaji wa kabila kwa kuizingira Gaza, kusababisha maelfu ya watu kuhama, na kulenga raia wasio na hatia.

“Hii si vita dhidi ya ugaidi — haya ni mauaji ya watu wasio na hatia,” alisema. “Hadi sasa, raia 62,000 wamepoteza maisha kutokana na mashambulizi ya Israel, kati yao angalau watoto 20,000. Watu 10,000 zaidi wako hawajulikani waplipo na wengine wapo chini ya vifusi.”

Yalcin aliituhumu Israel kuharibu asilimia 80 ya majengo ya Gaza, ikiwemo hospitali, shule, na misikiti, na kuwafukuza watu asilimia 90 ya wakazi wa ukanda huo. Alidai serikali za Magharibi zimefumba macho kwa ukatili huo kutokana na ushawishi wa vikundi vya kupigania maslahi ya Israel.

“Mauaji haya ya halaiki hayawezi tena kufichwa,” alisema. “Taasisi za kimataifa hazitekelezi wajibu wao, huku miji mingi ya Magharibi ikibaki mateka wa kampeni za Israel.”

Wito kwa Ulimwengu wa Kiislamu

Akihutubia jamii kubwa ya Waislamu, Yalcin aliwataka kuungana na kuwaonya kwamba ukosefu wa mshikamano na mgawanyiko utanufaisha maslahi ya Israel pekee.

“Simameni na ndugu zenu walioteswa. Mkishindwa kufanya hivyo, wale wanaoshambulia Gaza leo watakulenga wewe kesho,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya Wapalestina, Yalcin alisema Uturuki imewaletea “salamu za mamilioni ya watu pamoja na salamu za Rais Recep Tayyip Erdogan.”

“Tuko hapa kwa imani na mshikamano wetu wote. Tunaelewa upinzani wenu dhidi ya Israel na tunawaheshimu mashahidi wenu,” Yalcin aliwaambia wakaazi wa Gaza.

Nafasi na matakwa ya Uturuki

Yalcin alisisitiza kuwa Uturuki imekata kabisa uhusiano wa kisiasa, kiuchumi, na biashara na Israel na imekuwa ikiisaidia Gaza kwa misaada ya kibinadamu tangu mwanzo wa mgogoro.

Alirudia msimamo wa Ankara kwamba kusitishwa mapigano mara moja ni muhimu, ikifuatiwa na suluhisho la mataifa mawili lililotegemea mipaka ya mwaka 1967.

Alieleza matarajio ya Uturuki: kufungua Gaza kwa misaada ya kibinadamu, kuondoa marufuku ya kuingia, kuzuia uvamizi zaidi, kuanzisha mchakato wa amani wa haki, kufuatilia maafisa wa Israel kwa uhalifu wa kivita, na kuwajibisha Israel kwa ajili ya ujenzi upya kupitia fidia za vita.

“Yerusalemu ni qibla chetu cha kwanza (mwelekeo ambao Waislamu huelekea wakati wa sala), mahali ambapo Mtume alituwa kutoka safari ya mbinguni. Hata dunia ikiipa mgongo Gaza, Uturuki haitasita kupaza sauti yake dhidi ya ukandamizaji na mauaji haya ya halaiki,” alisema Yalcin.

Alimalizia kwa kusema kuwa ziara ya Uturuki Rafah ilikuwa ni kuleta kipaumbele cha hali ya Gaza kwa ulimwengu.

“Watu wa Gaza hawajasahaulika, na hawako peke yao,” alisema.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us