AFRIKA
3 DK KUSOMA
Mke wa rais wa Uturuki atembelea maonyesho ya wajasiriamali na wake wa viongozi
Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya umewaleta pamoja wake wa viongozi katika maonesho yajulikanayo kama "Safari ya mapishi ya ladha ya karne ya Anatolia", ambapo mke wa Rais wa Uturuki ameandamana na wageni na kutoka ufafanuzi wa bidhaa za asili.
Mke wa rais wa Uturuki atembelea maonyesho ya wajasiriamali na wake wa viongozi
Mke wa Rais wa Uturuki akitembelea maonesho ya "Culinary Journey to Anatolian Centenary Flavours" , akiongozana na wake wa viongozi wengine. /Picha: AA
2 Machi 2024

Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan ametembelea maonesho ya "Safari ya mapishi ya ladha ya karne ya Anatolia" pamoja na wake wa viongozi wengine waliohudhuria Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya.

Katika toleo lake la tatu, Mkutano umeleta pamoja viongozi wa nchi na serikali, mawaziri, wanadiplomasia, wafanyabiashara, wasomi, wabobezi, na majopo mbalimbali na maonesho yaliyohusisha masuala mbalimbali.

Mkutano huo ukiingia siku yake ya pili Jumamosi, umehodhi maonesho ya "Safari ya mapishi ya ladha ya karne ya Anatolia", ukitoa fursa kwa washiriki kuona bidhaa zenye alama ya kijiografia na bidhaa za mkono.

Mke wa Rais wa Uturuki ametembelea maonesho pamoja na Rais wa zamani wa Croatia Kolinda Grabar Kitarović, mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini (TRNC) Zerrin Ustel, mke wa rais wa TRNC Sibel Tatar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Grace Naledi Mandisa Pandor, na mke wa Rais wa Serbia Tamara Vucic.

Mke wa Rais wa Uturuki na viongozi alioandamana nao alitoa elimu kuhusu mavazi na vitu vyengine vya kitamaduni, pamoja na rangi.

Wageni pia walitembelea vibanda vinavyoonesha bidhaa za kijiografia zenye ithibati kutoka Umoja wa Ulaya, wakati mke wa Rais wa Uturuki akiandamana nao.

Mjumuiko huo umefanyika kama sehemu ya Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya, ukutoa fursa ya kubadilisha tamaduni kupitia kioo cha jiografia kwa vitu vya asili vilivyotengezwa.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us