MICHEZO
2 DK KUSOMA
Manchester City yatwaa taji la EPL kwa mara ya nne mfululizo
Manchester City imewafunga West Ham United 3-1 siku ya Jumapili na kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya nne mfululizo.
Manchester City yatwaa taji la EPL kwa mara ya nne mfululizo
Phil Foden and Rodri waliifungia Manchester City dhidi ya West Ham United, Mei 19, 2024. / Picha: Reuters
19 Mei 2024

Manchester City imetwaa taji la nne la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), na kuwa timu ya kwanza kushinda kombe hilo mfululizo.

Kikosi cha Pep Guardiola kiliwafunga West Ham United mabao 3-1 katika mchezo wao wa mwisho katika uwanja wa Etihad na kunyakua taji hilo, huku kukiwa na mchuano mkali kati yake na Arsenal, ambayo imeshika nafasi ya pili.

City wamekamilisha msimu wa 2023/24 wakiwa na pointi 91, mbili mbele ya Arsenal, na bado wako kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kombe la FA katika fainali dhidi ya wapinzani wao Manchester United kwenye Uwanja wa Wembley Jumamosi, Mei 25.

Msururu wa vikombe

Hili linakuwa taji la 10 la Ligi Kuu kwa Manchester City katika historia ya klabu hiyo, na la saba tangu wamiliki wao wa Abu Dhabi City Football Group wachukue timu ya Uingereza mwaka 2008.

Kwa sasa, Guardiola ameshinda mataji 17 ya dhahabu tangu ajiunge na City, mataji ambayo yanajumuisha sita ya Ligi Kuu, moja la Ligi ya Mabingwa, mawili ya Kombe la FA, manne ya Kombe la Ligi, moja la UEFA Super Cup, moja la Kombe la Dunia la Klabu ya FIFA na Ngao mbili za Jamii.

Sita bora Ligi Kuu ya Uingereza:

Manchester City – alama 91

Arsenal – alama 89

Liverpool – alama 82

Aston Villa – alama 68

Tottenham Hotspur – alama 66

Chelsea – alama 63

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us