MICHEZO
1 dk kusoma
Malkia wa Kenya wapata ushindi dhidi ya Vietnam kwenye voliboli
Timu ya Kenya ya voliboli imeshangaza Poland na Vietnam katika mashindano ya Kombe la Dunia la mchezo huo. Kenya ilionesha umahiri wake na kuwaduwaza zaidi Vietnam.
Malkia wa Kenya wapata ushindi dhidi ya Vietnam kwenye voliboli
Voliboli. / Reuters
tokea siku moja

Licha ya kuwa vinara wa mashindano ya barani Afrika wakiwa na mataji kumi, Malkia Strikers wamekuwa hawafanyi vizuri katika jukwaa la Dunia.

Siku ya Jumatano waliishinda Vietnam kwa seti 3-0 (25-23, 25-22, 25-18) kuwafanya wapate ushindi wao wa tatu katika mechi kumi walizocheza mashindano ya Dunia.

Walihitaji ushindi dhidi ya nchi zingine mbili ili waweke historia ya kuwa timu ya kwanza barani Afrika kufuzu kwa hatua ya pili ya mashindano hayo ya Dunia yanayofanyika kila baada ya miaka minne lakini hilo halikutimia kutokana na kushindwa kwenye mechi zao dhidi ya Ujerumani (3-0) na Poland (3-1) katika kundi ‘G’.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us