AFRIKA
2 DK KUSOMA
Armenia: Helikopta ya Waziri Mkuu yatua kwa dharura kufuatia hali mbaya ya hewa
Waziri Mkuu Nikol Pashinyan amesema kuwa tukio hilo limetokea karibu na eneo la Vanadzor, ambalo ni la tatu kwa ukubwa nchini Armenia.
Armenia: Helikopta ya Waziri Mkuu yatua kwa dharura kufuatia hali mbaya ya hewa
Kulingana na vyombo vya habari, Waziri Mkuu huyo alikuwa anaelekea katika eneo la makazi la Baganis kwenye mpaka na Azerbaijan./Picha: Reuters       / Others
25 Mei 2024

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan amesema siku ya Jumamosi kuwa helikopta yake ilitua kwa dharura kutokana na uwepo wa hali mbaya ya hewa.

Tukio hilo limetokea karibu na Vanadzor, mji wa tatu kwa ukubwa nchini humo na mji mkuu wa jimbo la Lori, aliandika Pashinyan kwenye ukurasa wake wa Facebook.

"Imebidi helikopta yetu itue kwa dharura katika eneo la Vanadzor kutokana na hali mbaya ya hewa.

Kwa sasa, tunaendelea na safari yetu kwa gari. Nawatika siku njema," alisema.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, waziri mkuu alikuwa akielekea kwenye makazi ya Baganis kwenye mpaka na Azerbaijan, ambapo mpaka huo uliwekwa hivi karibuni.

Tukio hilo linakuja wiki moja baada ya kutokea kwa ajali ya helikopta iliyomuua Rais wa Iran, Ebrahim Raisi na msafara wake.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us