MICHEZO
1 DK KUSOMA
Tanzania yaikaribisha Ethiopia ikisaka tiketi ya AFCON 2025
Taifa Stars inasaka tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON 2025 itakapocheza na Ethiopia katika mchezo wa kundi H utakaofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Tanzania yaikaribisha Ethiopia ikisaka tiketi ya AFCON 2025
Baadhi ya wachezaji wa 'Taifa Stars' wakiwa mazoezini kujiandaa na mchezo huo./Picha:TFF / Others
4 Septemba 2024

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars', inajitupa uwanjani Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, kumenyana na Ethiopia katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).

Mchezo huo wa Kundi H, ambalo pia linahusisha timu za DR Congo na Guinea utachezwa siku ya Septemba 4, 2024.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa Taifa Stars katika mashindano hayo ya kufuzu AFCON na baada ya kuikabili Ethiopia itasafiri hadi Ivory Coast kukabiliana na Guinea, Septemba 10.

Tanzania ilishiriki michuano ya AFCON 2024 iliyofanyika nchini Ivory Coast, ambapo waliambulia alama 1, katika kundi lililohusisha timu za Morocco, Zambia na DR Congo.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us