AFRIKA
2 DK KUSOMA
Ugonjwa wa Mpox bado haujadhibitiwa, Africa CDC yasema
Kauli hiyo inakuja wakati Rwanda imeanza kutoa chanjo ya ugonjwa huo kwa watu walio kwenye mazingira hatarishi.
Ugonjwa wa Mpox bado haujadhibitiwa, Africa CDC yasema
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC) kimesema kuwa bado ugonjwa wa Mpox haujadhibitwa barani Afrika./Picha: Reuters / Others
20 Septemba 2024

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC) kimesisitiza kuwa bado bala la Afrika halijaweza kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Mpox.

“Kwa sasa, tunaweza kusema kuwa bara la Afrika bado halijaweza kuudhibiti ugonjwa wa Mpox,” alisema Jean Kaseya, Mkurugenzi Mkuu wa Afrika CDC amesema katika mkutano wa mtandaoni.

Ukilinganisha na kipindi kama hiki kwa mwaka jana, Kaseya amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la asilimia 177 na 38.5 katika idadi ya maambukizi na vifo mtawalia, katika nchi 15 barani Afrika.

Kulingana na Kaseya, kumekuwepo na maambukizi mapya 2,912 katika wiki za hivi karibuni, na vifo 14, huku akisisitiza haja ya kuongeza na kuimarisha njia za uchunguzi na udhibiti wa ugonjwa huo.

Bara la Afrika lina jumla ya maambukizi 29,000 na vifo 738 mwaka huu, kwa mujibu wa Afrika CDC.

Kaseya, pia amegusia changamoto za uhaba wa vifaa vya kupimia ugonjwa huo.

Hata hivyo, ameonesha matumaini kuwa bara la Afrika litapokea dozi milioni 10 za ugonjwa huo kutoka kwa washirika wa afya ulimwenguni.

“Tuzungumzie chanjo. Tumeona mafanikio nchini Rwanda, ambako watu 500 wameshapata chanjo hiyo,” alisema Kaseya.

Rwanda imepokea dozi 1,000 za chanjo hiyo kutoka Nigeria chini ya mkataba wa nchi mbili, kutoka dozi 10,000 ambayo ilipokea kutoka Marekani.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us