AFRIKA
1 DK KUSOMA
Mawaziri wa Rwanda na DRC wakutana nchini Angola
Mawaziri hao wamefanya kikao chao cha tano katika mji mkuu wa Angola, Luanda.
Mawaziri wa Rwanda na DRC wakutana nchini Angola
Kikao hicho kinaungwa mkono na Umoja wa Afrika./Picha: @angola_Mirex      / Others
12 Oktoba 2024

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekutana tena nchini Angola kujadiliana namna ya kurejesha utulivu katika eneo la mashariki ya DRC.

Kikao hicho, ambacho kinaungwa mkono na Umoja wa Afrika, kilikuwa chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Tete António.

Mkutano huo, unaojulikana kama ‘mchakato wa Luanda’ uliasisiwa katikati ya mwaka 2022, kwa lengo la kumaliza uhasama wa kidiplomasia kati ya Rwanda na DRC uliotakana na vita kati ya jeshi la Congo na kikundi cha M23.

Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Thérèse Kayikwamba Wagner na mwenzake kutoka Rwanda Olivier Nduhungirehe wako katika mji mkuu wa Angola, Luanda kushiriki majadiliano hayo.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us