AFRIKA
2 DK KUSOMA
Wakenya wapewa siku ya mapumziko kupisha uapisho wa Kithure Kindiki
Serikali ya Kenya imepitisha Novemba 1, 2024 kuwa siku ya mapumziko ili kupisha kuapishwa kwa Kithure Kindiki kama Naibu Rais wa nchi hiyo.
Wakenya wapewa siku ya mapumziko kupisha uapisho wa Kithure Kindiki
Profesa Kithure Kindiki./Picha: Reuters   / Others
31 Oktoba 2024

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Kenya imetangaza Novemba 1, 2024 kama siku ya mapumziko ili kuruhusu zoezi la kumuapisha Kithure Kindiki kama Naibu Rais wa nchi hiyo.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Musalia Mudavadi, amesema uamuzi huo unatoa nafasi kwa wakenya kushuhudia tukio la kuapishwa kwa Naibu Rais mteule Kithuri Kindiki.

Zoezi la kumuapisha Profesa Kindiki linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi.

Mnamo Oktoba 17 mwaka 2024, bunge la Seneti la nchini Kenya lilipitisha kura ya kumuondoa madarakani aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua.

Hatua hiyo, ilimlazimu Rais William Ruto kumteua Waziri wa Mambo ya ndani wa nchi hiyo, Kithure Kindiki kuchukua nafasi ya Gachagua, kabla ya Mahakama kupinga uteuzi huo.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us