MICHEZO
2 DK KUSOMA
Timu ya taifa ya Uganda yafuzu AFCON 2025
'The Uganda Cranes' inakuwa timu ya pili kutoka Afrika Mashariki kufuzu michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), zitakazofanyika nchini Morocco.
Timu ya taifa ya Uganda yafuzu AFCON 2025
Uganda inakuwa timu ya pili kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kufuzu michuano hiyo mikubwa barani Afrika baada ya DRC, huku Tanzania ikisubiri kujua hatma yake siku ya Novemba 16, 2024, itakapovaana na Ethiopia./Picha: Wengine / Others
14 Novemba 2024

Timu ya Taifa ya Uganda, maarufu kama ‘The Uganda Cranes’ imefuzu kushiriki ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), ikiwa imebakiza mechi mbili kibindoni.

‘The Uganda Cranes’ ilijihakikishia tiketi ya AFCON 2025 baada ya Sudan Kusini kuifunga Congo kwa mabao 3-2 jijini Juba, siku ya Alhamisi.

Matokeo hayo, yanaifanya Congo kubakia katika nafasi ya tatu, ikiwa imejikusanyia alama 4, ikiwa haina uwezo wa kuzipiku Uganda na Afrika Kusini zenye alama 10 na 8 mtawalia.

Uganda inakuwa timu ya pili kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kufuzu michuano hiyo mikubwa barani Afrika baada ya DRC, huku Tanzania ikisubiri kujua hatma yake siku ya Novemba 16, 2024, itakapovaana na Ethiopia.

Hii inakuwa mara ya nane kwa Uganda kushiriki michuano ya AFCON, ikiwa imeshashiriki mwaka 1962, 1974, 1976, 1978, 2017 na 2019.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us