AFRIKA
2 DK KUSOMA
Viongozi wa Afrika washiriki katika Kongamano la Maendeleo Endelevu la Abu Dhabi
Kongamano la ADSW ni jukwaa la ngazi ya juu linalowakutanisha viongozi wa dunia ili kuendeleza ajenda ya kimataifa ya maendeleo endelevu.
Viongozi wa Afrika washiriki katika Kongamano la Maendeleo Endelevu la Abu Dhabi
Rais wa Kenya William Ruto atarajiwa kusaini mikataba ya uchumi kati ya UAE na Kenya. /Picha: Emirates 24/7 / Others
14 Januari 2025

Kongamano la Wiki ya Maendeleo Endelevu la Abu Dhabi (ADSW) 2025, likaloendeshwa chini ya uangalizi wa Rais wa UAE, Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan litawaleta pamoja wakuu wa nchi 13 na zaidi ya mawaziri na maafisa wa serikali 140 pamoja na wadau wa biashara na teknolojia.

Mkutano huo utaendelea kwa siku mbili, Januari 14 na 15, na utajumuisha vikao 34 vyenye wazungumzaji zaidi ya 70, vinavyolenga kukuza mazungumzo na ushirikiano katika kuendeleza maendeleo endelevu na kusukuma hatua shirikishi, zenye matokeo.

Viongozi wa nchi kutoka Afrika watakaoshiriki katika mkutano huo ni pamoja na: William Ruto, Rais wa Kenya; Bola Tinubu, Rais wa Nigeria; Paul Kagame, Rais wa Rwanda; Wavel Ramkalawan, Rais wa Shelisheli; Yoweri Museveni, Rais wa Uganda.

Hussein Mohamed, msemaji wa Ikuku ya Rais nchini Kenya, amesema kupitia mtandao wa X, kwamba Rais wa Kenya William Ruto atafanya mikutano na viongozi wakuu wa mataifa mbali mbali, akiwemo Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim.

Msemaji huyo wa Ikulu alisema majadiliano yatalenga katika kuimarisha ushirikiano katika nishati, biashara, uwekezaji na teknolojia, ambazo ni nguzo muhimu za Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi ya Kenya.

"Wakati wa ziara hiyo, Kenya na UAE zinatarajiwa kutia saini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi, ambao utakuza ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na maendeleo kati ya nchi hizo mbili," amesema.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika na mashirika ya habari
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us