AFRIKA
2 DK KUSOMA
Kenya yapeleka askari zaidi nchini Haiti
Kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen, shughuli ya ulinzi wa amani nchini inayofanywa na Kenya nchini Haiti, inazidi kukua ikiwa ni uthibitisho wa Kenya kwa jumuiya ya kimataifa.
Kenya yapeleka askari zaidi nchini Haiti
Idadi hiyo, inafikisha jumla ya askari polisi 744 waliotumwa nchini Haiti kwa ajili ya kupambana na magenge ya kihalifu yaliyokithiri nchini humo./Picha:  @AbdikadirNeema / Others
6 Februari 2025

Kenya imetuma askari wengine 144 nchini Haiti, kujaribu kulinda amani na kurejesha utulivu nchini humo.

Askari hao, ambao ni wanaume 120 na wanawake 24, wameelekea Haiti asubuhi ya Februari 6, 2025 baada ya kuagwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kipchumba Murkomen.

Idadi hiyo, inafikisha jumla ya askari polisi 744 waliotumwa nchini Haiti kwa ajili ya kupambana na magenge ya kihalifu yaliyokithiri nchini humo.

“Leo nimewaaga askari wengine 144 ili kuweza kuongeza nguvu kwa wenzao waliotangulia, na tayari tunaona maendeleo mazuri huko Haiti,” aliandika Murkomen katika ukurasa wake wa X.

Mbali na Kenya, nchi zingine, zikiwemo Guatemala na El Salvador, zimeongeza maaskari wao nchini humo ili kujaribu kudhibiti magenge ya wahalifu.

“Tunaendelea kuwasiliana Umoja wa Mataifa pamoja na nchi zinazounga mkono hatua ya kutuliza ghasia nchini Haiti, ikiwemo Marekani,” aliongeza Murkomen.

Kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen, shughuli ya ulinzi wa amani nchini inayofanywa na Kenya nchini Haiti, inazidi kukua ikiwa ni uthibitisho wa Kenya kwa jumuiya ya kimataifa.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us