tokea masaa 7
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) liko mbioni kuanza safari za Dar es Salaam hadi Lagos kufuatia kupewa kwa kibali maalumu kutoka serikali ya Nigeria.
Kulingana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya anga ya Nigeria, Ibrahim Abubakar Kana, kibali cha kuiruhusu Air Tanzania kutua nchini humo.
Kibali hicho kitarahisisha ufanisi, kuboresha usalama na kuongeza ushirikiano wa safari za anga kati ya Tanzania na Nigeria.
“Hii ni hatua muhimu katika ukuzaji wa ushirikiano wa safari za anga na itaongeza weledi zaidi katika eneo hilo,” alisema.
Kulingana na Kana, hatua hiyo inaendena na jitihada za Nigeria za kukuza utangamano wa kikanda na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara barani Afrika.
CHANZO:TRT Afrika Swahili