AFRIKA
2 dk kusoma
Misri inasema haitoacha haki ya maji yake huku kukiwa na mvutano kuhusu bwawa la Nile na Ethiopia
Rais wa Misri anasema suala la maji ya Nile ni madai ya sehemu ya shinikizo kuhusu malengo yasiyohusiana na suala hilo
Misri inasema haitoacha haki ya maji yake huku kukiwa na mvutano kuhusu bwawa la Nile na Ethiopia
tokea masaa 16

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amekataa hatua ya upande mmoja kuhusu Mto Nile, akionya kuwa yeyote anayeamini kuwa Misri itatelekeza haki za maji yake “amekosea.”

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni, Sisi anasema maji wanayopata kwa mwaka kutoka kwenye vyanzo vyote vya mito ya Nile ni kiwango cha bilioni 1,600, ambayo mengi yanapotea katika misitu, maeneo oevu, na kwenye ardhi.

“Ni kiwango kidogo ambacho kinafika Nile, na hiyo ni Misri na Sudan kwa pamoja wanapata bilioni 85 - ikiwa ni asilimia 4 ya idadi yote,” aliongeza.

Kiongozi huyo wa Misri alisisitiza kuwa kuiachia sehemu yao ya maji “kutamaanisha kuachia maisha ya Misri kabisa,” huku nchi ikikosa njia mbadala ya maji na kuwa na kiwango kidogo cha mvua.

Sisi anasema wakati Misri inaridhishwa na yanayoendelea kwa maslahi ya nchi jirani kufaidika na maji ya Nile – iwe kwa kilimo, uzalishaji umeme, au maendeleo kwa ujumla, “ Ukuaji kama huo hautakiwi kupunguza idadi ya maji kwa Misri.”

Mapema mwezi Julai, Ethiopia ilitangaza kukamilika kwa mradi wa bwawa kubwa kwa ajili ya maandalizi ya kulifungua rasmi mwezi Septemba.

Ujenzi wa bwawa hilo kubwa la Ethiopia (GERD) ulianza 2011. Kwa miaka kadhaa limekuwa tatizo la taharuki ya kidiplomasia, hasa kati ya Ethiopia, Sudan, na Misri, ambayo inahofia mgao wake wa Nile unaweza kupungua.

Licha ya majadiliano ya miaka kadhaa katika ngazi ya Muungano wa Afrika na wapatanishi wa kimataifa, nchi zote tatu bado hazijakubaliana kisheria kuhusu utaratibu wa usimamizi wa muda mrefu wa maji hayo.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us