AFRIKA
2 dk kusoma
Kocha McCarthy kubeba matumaini ya ‘Harambee Stars’?
Wingi wa mashabiki wanaojaza uwanja wa Moi Kasarani, ni ushahidi tosha wa imani kubwa waliyonayo kwa McCarthy na kikosi chake.
Kocha McCarthy kubeba matumaini ya ‘Harambee Stars’?
Kocha wa 'Harambee Stars' ya Kenya akiwa mazoezini./Picha: Wengine

Wakati wachezaji wa ‘Harambee Stars’ wakizidi kuneemeka kwa ahadi za Rais William Ruto, jina moja linatawala mafanikio ya timu hiyo ya taifa ya Kenya.

Toka atangazwe kuinoa ‘Harambee Stars’ mwezi wa tatu mwaka huu, ni wazi kuwa Benedict Saul McCarthy ameleta mabadiliko makubwa ndani ya kikosi hicho, ndani ya muda mfupi, tofauti na ilivyokuwa kwa watangulizi wake.

Ni ukweli usiopingika kuwa, nyota huyo wa zamani wa Porto ya Ureno, ameongeza ari ya ushindani na kujiamini ndani ya kikosi cha ‘Harambee Stars’.

Katika michezo saba aliyoiongoza timu ya taifa ya Kenya, McCarthy ameisadia timu hiyo kushinda 3, kutoa droo 3 na kupoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Gabon, na hivyo kurudisha matumaini ya mashabiki wa ‘Harambee Stars’ kwa timu yao ya taifa.

Awapo mazoezini au hata wakati wa mechi, kocha huyo hakupepesa macho, kwa yeyote yule aliyeonesha utovu wa nidhamu uzembe.

Kifupi, amekuwa mtu wa matendo na sio maneno tu.

Hii inadhihirishwa na uamuzi wake wa kujitoa kwenye mashidano maalumu ya CECAFA ya mataifa manne, yaliyokuwa yakifanyika nchini Tanzania, akioneshwa kutoridhishwa na miundombinu ya viwanja, kwa nia ya kuwalinda wachezaji wake kwa michuano ya CHAN 2024.

Raia huyo wa Afrika Kusini, ambaye anakiri kushawishiwa na nyota wa zamani wa Kenya, Mc Donald Mariga kuifundisha ‘Harambee Stars’, amefanikiwa kubadilsha mbinu za timu hiyo, akisisitiza umilikaji mpira, akibadilisha mfumo wa 4-2-3-1 hadi 4-2-4 ili kuharakisha mashambulizi.

Wingi wa mashabiki wanaojaza uwanja wa Moi Kasarani, ni ushahidi tosha wa imani kubwa waliyonayo kwa McCarthy na kikosi chake.

Je, McCarthy atafanikiwa kuipeleka Harambee Stars kwenye hatua ya Robo Fainali?

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us