AFRIKA
2 dk kusoma
Wanaoshukiwa kuwa waandamanaji wachoma jengo la serikali Afrika Kusini
Waziri wa Mambo ya Ndani Leon Schreiber anasema idara inakusanya ushahidi na itaandaa mashtaka ya jinai dhidi ya wale waliohusika
Wanaoshukiwa kuwa waandamanaji wachoma jengo la serikali Afrika Kusini
tokea masaa 14

Siku ya Jumanne waandamanaji wanadaiwa kuchoma moto jengo la ghorofa mbili la Wizara ya Mambo ya Ndani huko Germiston, katika mji wa Ekurhuleni karibu na Johannesburg, wakati wakipinga kuondolewa katika nyumba zao.

Waandamanaji walifunga barabara Germiston Jumanne asubuhi kupinga kuondolewa katika nyumba zinazomilikiwa na manispaa, ambapo inadaiwa wamekuwa wakiishi bila kulipa kodi.

"Tulipigiwa simu saa moja asubuhi za hapa na kugundua kuwa sehemu ya paa kwenye ghorofa ya kwanza la Wizara ya Mambo ya Nje limeporomoka," William Ntladi, Msemaji wa usimamizi wa majanga na dharura wa Ekurhuleni, aliwaambia waandishi katika eneo la tukio.

Alisema chanzo halisi cha moto huo bado hakijajulikana kufikia sasa. Hata hivyo, aliongeza kuwa itakuwa ni wahalifu, huku wengine wakidaiwa kutumia bomu la petroli kuchoma jengo hilo.

Ntladi anasema hakuna taarifa za majeruhi, lakini watu katika majengo ya karibu wametakiwa kuondoka.

Waziri wa Mambo ya Ndani Leon Schreiber alisema kwenye ujumbe mfupi kupitia X kuwa “Waziri wa Mambo ya Ndani inakusanya ushahidi kwa lengo la kuanzisha mashtaka ya uhalifu dhidi ya waliochoma jengo Germiston, ambao ulienea mpaka katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani.”

Polisi walitumia risasi za mpira kutawanya wakazi katika nyumba za Pharoe Park ambao walikuwa wanawarushia mawe wakiwa wameongozana na maafisa wa mahakama kuwaondoa katika makazi yao.

Wafanyakazi kutoka katika kampuni ya kuwaondoa watu katika makazi walionekana wakiwaondoa wapangaji kwa lazima na kuweka vifaa vyao nje. Kwa kawaida maandamano kama hayo nchini Afrika Kusini huwa yanageuka kuwa na vurugu, na waandamanaji wanaharibu miundombinu.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us