AFRIKA
1 dk kusoma
Morocco yafufua matumaini kwa kuifunga Zambia 3-1, huku DRC ikiizaba Angola 2-0
Mabingwa mara mbili wa mashindano ya wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani Morocco wamefufua matumaini yao kwenye michuano ya CHAN 2024 baada ya kuwabamiza Zambia 3-1 jijini Nairobi Alhamisi.
Morocco yafufua matumaini kwa kuifunga Zambia 3-1, huku DRC ikiizaba Angola 2-0
Timu ya Morocco. /CAF
tokea masaa 7

Magoli ya Mohamed Hrimat, Oussama Lamlaoui, na Sabir Bougrine yaliipa timu hiyo ushindi katika kundi A kwenye mechi iliyochezwa uwanja wa Nyayo, Nairobi na kuweka matumaini juu kwa simba hao kutoka milima ya Atlas baada ya kufungwa na wenyeji Kenya.

Matokeo hayo yamewaweka Morocco katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye kundi hilo.

Magoli ya Morocco kipindi cha kwanza

Morocco ilianza kwa malengo kabisa, ikifahamu kuwa ushindi utawapa nafasi nzuri ya kuendelea kubaki katika mashindano. Na wachezaji Khalid Aït Ouarkhane, Abdelhak Assal, na Youssef Mehri wote waliwakabili walinzi wa Zambia kwa lengo la kutafuta nafasi.

Walipata goli la kwanza katika dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza wakati kona ya Youssef Mehri ilipompata Mohamed Hrimat, ambaye aliingiza kimiani kufanya matokeo kuwa 1-0 wakati wa mapumziko.

Morocco walidhibiti mchezo huo vizuri, na kupiga mashuti kadhaa yaliyolazimisha mlinda mlango wa Zambia Francis Mwansa kuwa na kazi kubwa ya kuokowa.

Ushindi wa DRC

Katika mechi nyingine ya kundi hilo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) illifunga Angola 2-0 katika mechi iliyochezwa uwanja wa Kasarani, Nairobi.

Magoli ya DRC yalifungwa na Jephte Kitambala katika dakika ya 58, kabla ya Mokonzi Katumbwe kufunga kazi kwa chui wa DRC dakika ya 70.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us