AFRIKA
1 dk kusoma
Burkina Faso yapitisha sheria ya kuzuia mapenzi ya jinsia moja
Serikali ya Burkina Faso Jumatatu ilipitisha kwa kauli moja sheria inayozuia mapenzi ya jinsia moja kama sehemu ya mageuzi makubwa ya sheria za familia na uraia.
Burkina Faso yapitisha sheria ya kuzuia mapenzi ya jinsia moja
Nchi ya Mali ilipitisha sheria ya kuzuia mapenzi ya jinsia moja mnamo Novemba 2024. @CapitaineIb226/ / x
tokea masaa 17

Sheria hii mpya, inalingana na kampeni ya kuzuia mapenzi ya jinsia moja, inatoa adhabu ya kifungo cha hadi miaka mitano gerezani.

Mapenzi ya jinsia moto ni kinyume na sheria katika takriban nchi 30 za Afrika, kabla ya Burkina Faso kuchukua hatua hiyo.

"Wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja au vitendo vyengine vya aina hiyo watapigwa faini na kufungwa jela kati ya miaka miwili hadi mitano," alisema Waziri wa Katiba, Edasso Rodrigue Bayala, kupitia kituo cha taifa cha habari RTB.

Nchi jirani ya Mali, ambayo ni mshirika mkubwa wa Burkina Faso, nayo ilipitisha sheria kama hiyo mwezi Novemba 2024.

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us