AFRIKA
2 dk kusoma
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amfuta kazi mkuu wa majeshi baada ya miezi saba
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi wa nchi hiyo baada ya kuwepo kwa nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi saba tu na kumtaja mrithi wake.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amfuta kazi mkuu wa majeshi baada ya miezi saba
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi Julai 7, 2025./ Picha: AP
8 Julai 2025

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi baada ya kuwa kwenye nafasi hiyo kwa miezi saba tu na kumtaja mrithi wake, kulingana na matangazo katika redio ya taifa.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kumfuta kazi Paul Nang Majok katika matangazo yao ya Jumatatu usiku. Majok amekuwepo kwenye nafasi hiyo tangu mwezi Disemba. Katika matangazo hayo Kiir alimchagua Dau Aturjong kuwa mkuu mpya wa Majeshi.

Majok alikuwa anasimamia jeshi wakati wa mapigano na wapiganaji, wanaojumuisha zaidi vijana wa kabila la Nuer, na kusababisha mzozo wa sasa wa kisiasa.

"Kumekuwa na utamaduni kuwa unapoteuliwa, au kuhamishiwa majukumu haupewi sababu za kuteuliwa na hakuna haja ya kupewa sababu unapoachishwa kazi. Ni jambo la kawaida," amesema Lul Ruai Koang, Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini.

Machar yuko chini ya kifungo cha nyumbani

Sudan Kusini imekuwa katika amani rasmi na makubaliano ya amani tangu 2018 yaliyomaliza miaka mitano ya mapigano yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini machafuko kati ya jamii zinazozozana yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Mwezi Machi, Makamu wa Rais wa Kwanza Riek Machar aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani, kusababisha wasiwasi wa mapigano mengine.

Waziri wa habari Michael Makuei anasema kifungo hicho ni kutokana na Machar kuwasiliana na wanaomuunga mkono na "kuwataka wafanye uasi dhidi ya serikali kwa lengo la kutatiza amani ili kusiwe na uchaguzi Sudan Kusini na nchi iingie tena kwenye vita."

Chama cha Machar kimekuwa kikikanusha madai ya serikali kuwa wanaunga mkono wapiganaji, ambao wamekabiliana na jeshi kaskazini mashariki mwa mji wa Nasir mwezi Machi.

Mwezi Mei, jeshi la Sudan Kusini linasema limeudhibiti tena mji huo kutoka kwa wapiganaji hao wa White Army.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us