AFRIKA
1 dk kusoma
Zaidi ya 1,000 wafariki katika maporomoko ya ardhi katika kijiji cha Sudan Magharibi
Maporomoko ya ardhi yalitokea Agosti 31 baada ya siku kadhaa za mvua kunyesha, kundi linaloongozwa na Abdelwahid Mohamed Nour lilisema katika taarifa.
Zaidi ya 1,000 wafariki katika maporomoko ya ardhi katika kijiji cha Sudan Magharibi
Mvua kubwa imenyesha Magharibi mwa Sudan / Reuters
tokea masaa 10

Takriban 1,000 waliuawa katika maporomoko ya ardhi yaliyoharibu kijiji katika eneo la Milima ya Marra magharibi mwa Sudan, na kuacha mtu mmoja tu aliyenusurika, The Sudan Liberation Movement/Army ilisema Jumatatu.

Maporomoko ya ardhi yalitokea Agosti 31 baada ya siku kadhaa za mvua kunyesha, kundi linaloongozwa na Abdelwahid Mohamed Nour lilisema katika taarifa.

Vuguvugu hilo linalodhibiti eneo lililoko katika jimbo la Darfur, lilitoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya misaada kusaidia kurejesha miili ya wahanga wakiwemo wanaume, wanawake na watoto.

Kijiji "sasa kimesambaratika kabisa ," vuguvugu liliongeza.

Huku wakikimbia vita vikali kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika jimbo la Darfur Kaskazini, wakaazi walitafuta hifadhi katika eneo la Milima ya Marra ambako chakula na dawa hazitoshi.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili vimewaacha zaidi ya nusu ya watu wakikabiliwa na hali mbaya ya njaa na kuwafukuza mamilioni ya watu kutoka makwao huku mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, Al-Fashir, ukikabiliwa na mashambulio mabaya.

CHANZO:Reuters
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us