AFRIKA
1 dk kusoma
Jaji Mkuu wa Ghana Gertrude Torkornoo afutwa kazi kwa matumizi mabaya ya mamlaka
Rais wa Ghana John Mahama amemfuta kazi Jaji Mkuu wa nchi hiyo Gertrude Torkonoo baada ya uchunguzi kubaini madai ya matumizi mabaya ya mamlaka yake.
Jaji Mkuu wa Ghana Gertrude Torkornoo afutwa kazi kwa matumizi mabaya ya mamlaka
Gertrude Torkornoo amekuwa jaji mkuu wa Ghana tangu 2023. / Ghana News Agency
tokea masaa 9

Rais wa Ghana amemfuta kazi Jaji Mkuu wa nchi baada ya uchunguzi kubaini madai ya matumizi mabaya ya mamlaka.

Gertrude Araba Esaaba Sackey Torkonoo, 61, mwanamke wa tatu kuongoza mahakama kuu ya Ghana, alisimamishwa kazi katika nafasi yake hiyo aliyoingia 2023 baada ya malalamiko kadhaa kuwasilishwa dhidi yake.

Rais John Mahama aliteua tume ya wajumbe watano ikiongozwa na jaji mwingine wa mahakama ya juu kuchunguza madai hayo, ikiwemo yale ya kuwepo kwa rekodi za uwongo za mahakama na ubadhirifu wa fedha za umma.

Tume hiyo ilibaini kuwa madai hayo "yalikuwa ya kweli na kupendekeza aondolewe ofisini ," taarifa kutoka ofisi ya rais ilisema siku ya Jumatatu.

Mara ya kwanza kwa jaji mkuu kuondolewa ofisini Ghana

"Rais John Dramani Mahama ...amemfuta kazi Jaji Mkuu … kuanzia sasa hivi," taarifa ilisema.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa jaji mkuu aliye ofisini Ghana kuchunguzwa na kuondolewa ofisini.

Mahama, ambaye aliingia uongozini Januari 2025, ameapa kukabiliana na ufisadi nchini humo.

Haijafahamika mara moja kama Torkonoo atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us