AFRIKA
1 dk kusoma
"Afrika inaweza kulisha dunia nzima," asema Rais wa Senegal
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, siku ya Jumatatu alisema kuwa Afrika inaweza kulisha dunia nzima, akisisitiza kuwa vijana lazima wawe kiini cha mageuzi ya kilimo.
"Afrika inaweza kulisha dunia nzima," asema Rais wa Senegal
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye / / AA
2 Septemba 2025

Rais Faye aliyasema hayo katika mkutano wa kimataifa wa usalama wa chakula uliofanyika Dakar nchini Senegal na kuongeza kuwa, asilimia 65 ya ardhi inayofaa kwa kilimo duniani, na vijana wabunifu, na rasilimali nyingi ziko barani Afrika.

Rais Faye alihimiza Afrika ijitegemee yenyewe kufanikisha usalama wa chakula na kuchukua mtazamo wa kutafuta suluhisho, akisema hilo linahitaji uwekezaji mkubwa katika usimamizi wa maji, ubunifu, usindikaji wa mazao ndani ya nchi, na biashara kati ya nchi za Afrika.

Katika mkutano huo wa kila mwaka, Rais wa Rwanda Paul Kagame amelitaka bara la Afrika kuacha kutegemea dunia katika kila kitu na kusisitiza kwamba, bara hilo linaweza kujitegemea kwa sababu lina utajiri wa rasilimamali zote.

"Tunahitaji kuacha kuzungumza tu na tuanze kutenda. Vijana pia wanapaswa kuchukua hatua na kulinganisha madai yao na vitendo halisi," aliongeza Kagame.

Rais Kagame aliyasema hayo katika mkutano wa Africa Food Systems Forum jijini Dakar, Senegal, utakaoendelea hadi Septemba 5, ambao unalenga kuwaleta pamoja wadau mbalimbali ili kukuza mifumo ya kilimo endelevu na jumuishi barani Afrika.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us