Kamati ya Maandalizi ya Kenya (“LOC”) pamoja na Serikali ya Kenya wamethibitisha Maeneo sita rasmi ya Mashabiki jijini Nairobi kwa ajili ya mechi ya Kenya ya Kundi A kwenye michuano ya TotalEnergies African Nations Championship (“CHAN”) PAMOJA 2024 dhidi ya Zambia Jumapili, 17 Agosti.
Mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa Kasarani saa Tisa Alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.
Kamati iyo andalizi imetangaza maeneo sita yatakayotumiwa kuonyesha mechi jijini Nairobi.
Bustani Ya Uhuru, Lucky Summer, - Ngomongo (nyuma ya Uwanja wa Kasarani) Uwanja wa Dandora Utalii Stima Club, Viwanja vya Jacaranda, Viwanja vya Kibera DC.
Serikali ya Kenya, ikifanya kazi kwa karibu na Kamati ya Maandalizi ya Ndani, Shirikisho la Soka la Kenya ("FKF") na CAF wameanzisha hatua zilizoimarishwa ikiwa ni pamoja na:
Usalama ulioimarishwa katika vituo vya ukaguzi
Kuchanganua tikiti kwa uthibitishaji
Itifaki za kugundua tikiti ghushi
Kuongezeka kwa usalama ndani na karibu na Viwanja
Mashabiki walio na tikiti halali za mechi ya Kielektroniki pekee ndio wataruhusiwa kuingia katika uwanja wa Kasarani, huku mashabiki wasio na tikiti wakihimizwa kuzuru Maeneo hayo ya Mashabiki yaliyotengwa.
Kenya imejikuta lawamani mara kadhaa baada ya mechi kwa kupigwa faiani kubwa na CAF kutokana na utovu wa nidamu wa mashabiki wake pamoja na kuvunjwa itifaki na kuhatarisha maisha ya watu uwanjani kwa mkanyagano.
CAF imeitoza Kenya zaidi ya dola elfu 60 kufikia sasa kulingana na sera ya nidhamu ya uwanjani.
Pia Kenya imepokea onyo kali kuwa ikiwa tabia hii haikukomeshwa basi watalazimika kuhamishiwa mechi zao hadi maeneo mengine na mashabiki kufungiwa nje.
Mechi ijayo ya Kenya dhidi ya Zambia Jumapili ni muhimu kwani iwapo Kenya itashinda, itajithibitishia uongozi wa Kundi lao la kifo, Kundi A. Hata hivyo kufuatia mechi za Morocco kuifunga Zambia 3-1 na DRC kuifunga Angola 2-0.
Liwalo ni liwe, timu hiyo ya Afrika Mashariki imeshajikatia tikiti a robo fainali, ikiwa ndio mara ya kwanza kushiriki na kupenya.