AFRIKA
2 dk kusoma
Afrika Kusini yaeleza ripoti ya Marekani kuhusu haki kuwa 'siyo sahihi
Afrika Kusini imeielezea ripoti hiyo "kuwa na mapungufu" ambayo Marekani inasema hali ya haki za binadamu Afrika Kusini "imekuwa mbaya" , siku chache baada ya serikali ya Trump kuiwekea ushuru wa asilimia 30 kwa bidhaa zao nyingi wanazouza nje.
Afrika Kusini yaeleza ripoti ya Marekani kuhusu haki kuwa  'siyo sahihi
Afrika Kusini imeshtumu ripoti ya Marekani inayoieleza kuwa hali yake ya haki za binadamu "inakuwa mbaye." / Picha: Reuters
tokea masaa 21

Afrika Kusini imeitaja ripoti ya Marekani inayozungumza kuhusu hali ya haki za binadamu "kuwa na mapungufu", siku chache baada ya uongozi wa Donald Trump kuiwekea ushuru wa asilima 30 kwa bidhaa nyingi ambazo wanauza nje ya nchi.

Katika ripoti yake ya haki za binadamu ya kila mwaka iliotolewa siku ya Jumanne, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeishtumu Afrika Kusini kwa kuchukuwa "hatua za kutia hofu katika suala la kuchukuwa ardhi za jamii ya Waafrikaner na ukiukwaji wa haki kwa jamii za walio wachache."

Ikiwa wamewekewa ushuru mkubwa zaidi wa Marekani kuliko nchi yoyote Kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Kusini imekuwa ikilengwa na Trump, ambaye ameshtumu sheria za nchi hiyo za ardhi na zile za ajira ambazo ni kwa ajili ya kutatua usawa wa watu wa rangi tofauti.

Wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini ilijibu siku ya Jumanne ikieleza "kusikitishwa sana" na ripoti hiyo ya Marekani.

'Siyo sahihi na yenye mapungufu'

"Tumegundua ripoti hiyo siyo sahihi na ina mapungufu na imeshindwa kuakisi ukweli wa demokrasia wa katiba yetu," ilisema.

Sheria iliyotiwa saini mwaka huu na Rais Cyril Ramaphosa na kushutumiwa na Trump inaruhusu kuchukuliwa kwa ardhi bila fidia katika mazingira fulani.

Umiliki wa ardhi bado ni suala tata nchini Afrika Kusini, huku sehemu kubwa ya ardhi ikiwa bado inamilikiwa na wazungu miongo mitatu baada ya kumalizika kwa utawala wa ubaguzi kwa misingi ya rangi.

Afrika Kusini inatarajia kufikia makubaliano na Marekani, mshirika wake wa tatu kwa ukubwa kibiashara, ili kuokoa maelfu ya ajira katika sekta ya kilimo, magari na ya kutengeneza nguo ambazo zinategemea zaidi soko la Marekani.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us