Mkuu wa Umoja wa masuala ya haki za binadamu siku ya Jumatano alieleza kughadhabishwa kwake kwa mashambulizi makubwa ya wapiganaji wa RSF katika mji wa El Fasher na kambi ya karibu ya Abu Shouk, ambayo yamesababisha raia kadhaa kuuawa.
Taarifa za awali za ofisi ya haki za binadamu zinaonesha raia wasiopungua 57 wameuawa katika shambulizi hilo la Jumatatu, ikiwemo wakimbizi wa ndani 40 katika kambi ya Abu Shouk. Ofisi hiyo pia inafwatilia madai ya mauaji ya wakimbizi wakati wa mashambulizi hayo, ilisema katika taarifa.
"Tumesikitishwa tena na ukatili uliofanywa kwa raia huko El Fasher, ambao kwa mwaka mzima wamekuwa kwenye matatizo, wakishambuliwa na hali mbaya zaidi kwa watu," Volker Turk amesema. "Mashambulizi haya ya mara kwa mara kwa raia, ambayo yantia hofu kulingana na sheria ya kimataifa kuhusu haki za watu, hayakubaliki na lazima yasitishwe."
Kati ya Januari na Juni, kambi ya Abu Shouk ilishambuliwa vibaya na RSF, na kusababisha mauaji ya wakimbizi wa ndani 212 pamoja na kujeruji wengine 111, taarifa ilisema.
"Kwa mara nyingine tena, natoa tahadhari imetolewa kuhusu hatari ya mateso yanayochochewa kwa misingi ya kikabila huku RSF ikijaribu kuchukuwa udhibiti wa mji wa El Fasher na kambi ya Abu Shouk," Turk amesema.
Ametaka hatua za kuwalinda raia zichukuliwe, mapigano yasitishwe, na kutoa njia kwa raia kwenda maeneo mengine, akitoa wito kwa mataifa mengine kutumia uwezo wao na kumaliza mapigano hayo, huku akisisitiza kuwa "uwajibikaji ni muhimu kumaliza vurugu hizi."
Kufikia sasa, katika majimbo 18 ya Sudan, wapiganaji wa RSF wanadhibiti baadhi ya sehemu za Kaskazini na Magharibi mwa Kordofan, maeneo ya Kusini mwa Kordofan na majimbo ya Blue Nile, pamoja na majimbo manne kati ya matano ya eneo la Darfur.