Mwezi uliopita, China imezindua mipango ya kuwepo kwa bodi ya dunia kusimamia akili mnemba kwa lengo la ufikiwaji wa tekonolojia, ushirikiano wa maeneo ya mipakani, na hatua za kuondoa vizuizi.
Miezi sita kabla, nchini 58 zilikutana mjini Paris kuidhinisha azimio la “ujumuishaji na AI endelevu,” ambalo Marekani na Uingereza walikataa kutia saini.
Mitazamo inakuwa tofauti, lakini mfumo ni ule ule. Kuwania kudhibiti AI kunaenda kwa kasi kuliko juhudi za kuratibu.
Akili Mnemba ni msukumo katika uchumi, mifumo ya usalama.
Mifumo ya kuratibu ya sasa imetengenezwa kuimarika taratibu na kuwa na majukwaa mahsusi. Haikutengenezwa kuwa na kiwango cha uwezo wa binaadamu, kuchanganua picha za satelaiti ndai ya sekudne kadhaa, au kuratibu mashine.
Mafanikio ya Akili Mnemba, na mifumo inasisitiza mtazamo wa kuwa nyuma zaidi kimkakati.
Kwa kuangalia, udhibiti wa silaha au mipango ua ushirikiano kunaweza kufanya kuwe na kipimo cha kuepuka ushindani wenye utata. Kwa kifupi, makubaliano kama haya ni nadra.
Mifumo ya uratibu iliyofeli, kutoaminiana, na matumizi ya AI yanafanya makubaliano yaliyopita kuhusu silaha kushindwa kutimizwa hii leo.
Huku kukiwa na mipaka ya nchi, uratibu unawezekana kwa nchi ambazo zina taasisi ambazo ziko imara.
Serikali
Katika mazingira ya nchi, serikali zina uwezo. Mabunge yanaweza kupitisha sheria, wanaodhibiti wanaweza kutoa maagizo ya utekelezaji wa sheria, na taasisi zinaweza kulazimisha kuheshimiwa kwa sheria kwa wale wanaofanya kazi ndani ya mipaka yao.
Ili kuwa na udhibiti kamili kunahitaji kuwepo kwa miundombinu ya kiufundi, wadhibiti wanaoelewa mifumo, na taasisi imara kabisa zinazoendana na sheria na kubadilika kwa mifumo ya teknolojia.
Bila utaratibu huu itakuwa hakuna mtazamo wenye tija.
Bila watu wenye utaalamu, hata sheria bora za Akili Mnemba zitaishia tu kwenye karatasi.
Kutokuwa na sheria kali kunaondoa usiri, kunafanya mifumo itumike vibaya na kudhoofisha usalama wa taifa. Kuwa na mipango sahihi kunahitaji taasisi zenye uwezo, utashi wa kisiasa na kuendelea kuainisha. Wengine wataweza; wengine watashindwa.
Maadili ya Kimataifa
Taswira kimataifa ni mbaya zaidi. Sababu kuu ni mkakati. Akili Mnemba inaahidi uthabiti katika jeshi, na hakuna nchi yoyote yenye uwezo ambayo inataka kubaki nyuma.
Nchini Marekani pekee, matumizi katika sekta ya ulinzi yanakadiriwa kuwa karibu dola bilioni 2 kwa mwaka, huku mabilioni zaidi yakitumika kwenye majukwaa mengine. Bajeti hizi hazitarajiwi kusitishwa.
Sababu moja ya makubaliano ya silaha za nyuklia yamefanya kazi ni kutokana kuwa silaha zenyewe ni kubwa, haziwezi kufichwa na ni rahisi kuhesabu.
Mifumo ya AI haiko hivyo. Inaweza kufanyia mazoezi kwa siri, na kufichwa isionekane.
Hii inamaanisha makubaliano ya ‘kijeshi ya AI’ yatagusa tu teknolojia ya raia, jambo ambalo nchi nyingi hazitaki kuacha hilo wazi kwa ukaguzi kutoka mataifa ya nje.
Hali ya Kimataifa inatatiza mambo zaidi. Diplomasia yenyewe inapitia changamoto katika masuala yenye utata kama malengo ya mambo ya hali ya hewa, mabadiliko ya WTO, na kuzuia mauaji ya halaiki.
Uaminifu miongoni mwa mataifa yenye uwezo ni mdogo.
Mataifa yenye uwezo mkubwa wa AI, kama vile Marekani na China, wanaona hatari zaidi kuliko faida kujiwekea ukomo wenyewe.
Matokeo yake ni mazingira ya kusambaratika kwa jamii ya kimataifa. Mataifa yataendeleza mifumo yake ya silaha zinazowezeshwa na AI na mifumo ya kiintelijensia bila makubaliano na wengine.
AI itaendelea kuimarika, ikisaidiwa na fursa za kibiashara na usalama wa taifa. Udhibiti utadumaa, na pengo hili litajazwa na makubaliano mbali mbali.
Zama za AI zitakuwa hazina usawa. Mataifa kadhaa yataanzisha mifumo ambayo inaweka mizania ya ubunifu na usalama na uhuru wa nchi.
Kimataifa, mipango itaendelea bila kudhibitiwa, na mara moja moja kukiwa na makubaliano katika mazingira ya hatari zaidi.