MICHEZO
1 dk kusoma
Kipa Mbrazil Ederson ajiunga na Fenerbahce ya Uturuki akitokea Manchester City
Ederson amehitimisha safari yake ya mafanikio ndani ya City iliyoanza mwaka 2017.
Kipa Mbrazil Ederson ajiunga na Fenerbahce ya Uturuki akitokea Manchester City
Aliyekuwa kipa wa Manchester City, Ederson./Picha:Getty
2 Septemba 2025

Kipa wa Manchester City Ederson, amekamilisha uhamisho wake kuelekea klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki.

Hayo yanajiri wakati mtaliano Gianluigi Donnarumma akijiandaa kwenda kuchukua nafasi ya Ederson ndani ya Manchester City kwa dau la Dola Milioni 41, baada ya kuambiwa kuwa ‘hahitajiki tena’ na klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa, licha ya kuisaidia kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Kwa upande mwingine, City ilimnunua golikipa wa Burnley, James Trafford mwishoni mwa msimu, licha ya muingereza huyo kushindwa kuonesha makali yake.

Kuwasili kwa Donnarumma ndani na Manchester City, kulimpa nafasi Ederson kuhamia nchini Uturuki, akihitimisha safari yake ya mafanikio ndani ya City, ambayo ilianza mwaka 2017.

Katika taarifa yake, City ilimuelezea Ederson "kama mchezaji mwenye mafanikio makubwa katika historia ya klabu hiyo".

Ederson alikuwa ni sehemu ya kikosi cha Manchester City kilichoshinda mataji nane ya Ligi Kuu ya EPL pamoja na mawili ya FA.

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us