AFRIKA
1 dk kusoma
Rwanda kuzindua teksi za hewani zinazojiendesha zenyewe
Mpango huu unaimarisha nafasi ya Rwanda kama kitovu cha Afrika cha majaribio ya teknolojia ya kisasa ya anga, ilisema serikali ya nchi hiyo.
Rwanda kuzindua teksi za hewani zinazojiendesha zenyewe
Teknolojia ya teksi ya hewani inayojiendesha imevumbuliwa Rwanda / picha: Reuters
tokea masaa 5

Serikali ya Rwanda, kwa ushirikiano na Shirika la Barabara na Madaraja la China (CRBC), inaanza safari ya kwanza kabisa barani Afrika ya teksi za ndege za kielektroniki zinazojiendesha zenyewe.

Uvumbuzi umefanyika katika Mkutano wa Kilele wa Aviation Africa 2025, unaofanyika Kigali kuanzia Septemba 4-5.

Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Miundombinu ya Rwanda EHang, kampuni ya teknolojia ya usafiri wa anga ya mijini, imeshirikiana na CRBC kupanua uwepo wake katika soko la kimataifa kwa ajili ya kuzindua kwa mafanikio safari ya kwanza kabisa ya ndege yake ya EH216-S ya kuruka na kutua ya kielektroniki (eVTOL) barani Afrika.

"Rwanda inajenga mustakabali ambapo miji yetu ambayo imeunganishwa zaidi na uchumi wetu unaimarika zaidi kupitia ubunifu wa usafiri," Waziri wa Miundombinu, Jimmy Gasore, alinukuliwa akisema katika taarifa hiyo.

Mpango huu unaimarisha nafasi ya Rwanda kama kitovu cha Afrika cha majaribio na kutekeleza teknolojia ya kisasa ya anga, Wizara hiyo imesema.

Serikali ya Rwanda imeongeza kusema kuwa kwa kushirikiana na utaalamu wa kimataifa wa uhandisi wa CRBC, Rwanda inalenga kujenga mfumo mpya wa ikolojia wa usafiri wa angani (AAM), teknolojia iliyoundwa ili kupunguza msongamano wa magari, kuunganisha jamii, na kuunda chaguo endelevu za usafiri.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us