Gavana wa Benki Kuu ya Ethiopia Mamo Mihretu alisema Jumatano kuwa anaacha kazi, baada ya kuiongoza Benki hiyo kupitia mageuzi ya kina ya uchumi ikiwa ni pamoja na mzunguko wa sarafu ya birr.
Waziri Mkuu Abiy Ahmed alimteua Mamo kuwa Gavana wa Benki ya Taifa ya Ethiopia, NBE mnamo Januari 2023.
Haikuweza kufahamika mara moja iwapo amejiuzulu kwa hiari au ameshurutishwa.
Katika ujumbe wa kumuaga, Mamo alisema anaacha utumishi wa umma "ili kufanya fursa nyengine na kukabiliana na changamoto nyengine," akielezea wakati wake serikalini kama "heshima na chanzo cha kuridhika."
Chini ya uongozi wa Mamo, NBE ilianzisha uhuru zaidi, ilifungua sekta ya fedha kwa benki za kigeni, na kupata dola bilioni 10.5 za ufadhili wa nje, Mamo alisema katika taarifa yake kwenye X.
Tangu aingie madarakani mwaka wa 2018, Abiy amekuwa akijaribu kuukomboa uchumi wa Ethiopia ambao hadi sasa unadhibitiwa vikali. Ofisi ya Waziri Mkuu haikujibu maombi ya maoni.
Wakati wa ugavana wake, Mamo alianzisha mfumo wa sera ya kisasa ya fedha.
Alivumbua mfumo wa viwango vya kubadilisha fedha unaotegemea soko, na kusaidia kupitisha sheria ambayo iliimarisha uhuru wa benki kuu.
Pia alisimamia kufunguliwa kwa sekta ya fedha ya Ethiopia kwa benki za kigeni, kupanua ujumuishaji wa kifedha wa kidijitali, na kupata dola za Kimarekani bilioni 10.5 katika ufadhili wa nje kutoka kwa washirika wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia.
Mamo anaondoka serikalini baada ya miaka saba katika majukumu mbalimbali.
ili kufuata matamanio mengine na kukabiliana na changamoto nyingine, alisema.