tokea masaa 13
Dechan Moussavou aliipa timu yake ya Jamhuri ya Congo goli katika dakika ya 19 na kuwashangaza wengi, lakini Joseph Layousse akawasawazishia Simba wa milima ya Teranga katika kipindi cha pili kwenye uwanja wa Amaan.
Kwa matokeo hayo sasa Senegal wana alama nne baada ya mechi mbili, huku Congo ikiwa na alama mbili.
Zilizopendekezwa
Goli la Congo la dakika ya 19, lilipigwa vizuri kutoka kwa Charles Atipo na kumfikia Dechan Moussavou ambaye bila kusuasua akaipachika wavuni kwa karibu.
Timu zote mbili zilionekana kupimana nguvu, licha ya Senegal kupewa nafasi kubwa ya kushinda mechi hiyo.
CHANZO:TRT Afrika Swahili