AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Salva Kiir awafukuza kazi mawaziri wake watatu
Taifa hilo, ambalo lilijitenga kutoka Sudan mwaka 2011, limekumbana na hali ya machafuko kufuatia kuhasimiana kati ya Kiir na Naibu wake, Riek Machar uliopelekea kuanzishwa kwa makubaliano ya kugawana madaraka, mwaka 2018.
Rais Salva Kiir awafukuza kazi mawaziri wake watatu
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini./Picha:Wengine
tokea masaa 8

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amewaachisha kazi mawaziri wake watatu, akiwemo na gavana wa jimbo la magharibi la Bahr el Ghazal, katika mabadiliko aliyoyafanya kwenye baraza lake la mawaziri siku ya Jumatatu.

Kupitia tamko take lililorushwa na Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC), Salva Kiir amemfuta kazi Waziri wake wa Sheria Wek Mamer Kuol na kumteua Joseph Geng Akec kama mbadala wake.

Katika hatua hiyo hiyo, Kiir amemteua Mary Nawai kama Waziri wa Vijana na Michezo, akichukua nafasi ya Akec.

Rais Kiir, pia alimuachisha kazi Naibu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Mapato ya Sudan Kusini Taban Abel Aguek, nafasi yake ikichukuliwa na John Malek.

Hata hivyo, hakuna sababu zozote zilizotolewa kufuatia maamuzi hayo ya Rais Kiir.

Taifa hilo, ambalo lilijitenga kutoka Sudan mwaka 2011, limekumbana na hali ya machafuko kufuatia kuhasimiana kati ya Kiir na Naibu wake, Riek Machar uliopelekea kuanzishwa kwa makubaliano ya kugawana madaraka mwaka 2018.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us