AFRIKA
1 dk kusoma
Ghana inaonya kuhusu kukatika kwa umeme Jumapili wakati wa kuimarisha mifumo
Ghana imeonya kuwa umeme utakatwa Jumapili, wakati mifumo ya usambazaji itakapokuwa inaimarishwa.
Ghana inaonya kuhusu kukatika kwa umeme Jumapili wakati wa kuimarisha mifumo
Ghana inatarajia uimarishwaji wa mifumo Julai 13, 2025 kutaongeza upatikanaji wa umeme. / Picha: Reuters
9 Julai 2025

Kampuni ya nishati ya Italia ya Eni itasitisha huduma zake kwa muda siku ya Jumapili nchini Ghana ili waimarishe mifumo ya usambazaji, na huenda wakasababisha kukatika kwa umeme, nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilisema siku ya Jumatano.

Ghana, nchi ya pili kwa uzalishaji mkubwa wa kakao duniani, imekuwa ikijaribu kuimarisha uzalishaji wake wa mafuta na gesi ili kuongeza mapato ya nchi.

Imefikia makubaliano na kampuni ya Eni kuongeza usambazaji wa gesi kwa futi milioni 30 kwa siku hadi milioni 270, waziri wa nishati alisema katika taarifa kwenye mtandao wa X Jumatano.

Ili kutimiza uimarishwaji, Eni itasimamisha kwa muda operesheni zake, kusababisha "kutokuwepo kwa uzalishaji wa gesi kwa ajili ya umeme," taarifa hiyo ilisema.

'Umeme kukatika'

Akizungumza katika hafla moja siku ya Jumatatu katika mji wa kusini wa Kumasi, Waziri wa Nishati John Jinapor alisema kuna uwezekano Ghana "umeme ukakatika" wakati mtambo huo utakapokuwa haufanyi kazi.

"Kazi hiyo itakapokamilika, tutakuwa na usambazaji mzuri wa gesi, kuongeza uzalishaji wa gesi na hiyo itaimarisha usambazaji wa umeme," alisema.

Wiki iliopita, kampuni ya Tullow Oil ilisema katika taarifa kuwa inapanga kuongeza usambazaji wa gesi hadi futi milioni 130 kwa siku.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us