7 Agosti 2025
Kocha wa Harambee Stars Benni McCarthy anasema watakuwa makini wakati watakapokabiliana na Angola kwenye mechi ya kundi ya A, huku wakiwa tayari wametia alama tatu kibindoni.
Timu ya Angola, ambayo iko katika nafasi ya 85 katika orodha ya Shirikisho la Soka duniani FIFA, ikilinganishwa na Kenya, ambayo iko katika nafasi ya 109, na inabidi wakabiliane vilivyo kuepuka wasipoteze fursa ya kufuzu kwa hatua ya muondoano.
Ushindi kwa Harambee Stars hakutowapa zawadi ya fedha zaidi ya dola 7,000 kutoka kwa Rais William Ruto lakini kutawasogeza karibu kufuzu kwa hatua nyingine.