MICHEZO
1 dk kusoma
Uganda yapiga marufuku vuvuzela na firimbi wakati wa michuano ya CHAN 2024
Polisi pia wamepiga marufuku mashabiki kuingia uwanjani na vitu kama nyundo, miamvuli, mifuko mikubwa kamera za video na chupa za chai.
Uganda yapiga marufuku vuvuzela na firimbi wakati wa michuano ya CHAN 2024
Wachezaji wa Uganda Cranes wanacheza tena 8 Agosti./Picha: Wengine / Others
tokea masaa 4

Huduma ya Polisi nchini Uganda imetoa masharti mapya kwa mashabiki wakati wa michuano ya kikanda ya soka ya CHAN 2024 ambayo inafanyika katika uwanja wa Taifa wa Mandela , namboole nchini humo.

“ Ili kuhakikisha matumizi salama na ya kufurahisha kwa kila mtu, bidhaa zifuatazo haziruhusiwi kabisa ndani ya majengo ya uwanja: vuvuzela, filimbi, chupa za glasi, na makopo na fataki.” imesema katika taarifa.

Inasema kuwa ilifanya mkutano wa pamoja na kamati ya kuandaa michuano hiyo nchini, na wawakilishi wa shirkisho la soka la CAF, kwa ajili ya kuimarisha usalama kwa michezo zilizosalia.

Polisi pia wamep[iga marufuku mashabiki kuingia uwanjani na vitu kama nyundo, miamvuli, mifuko mikubwa kamera za video na chupa za chai.

Ijumaa 8 Agosti 2025, uwanja wa Taifa wa Mandela utakuwa mwenyeji wa mechi baian ya Algeria na Afrika Kusini mwendo wa saa kuni ma moja jioni.

Guinea itapambana na Timu ya Taifa ya Uganda katika uwanja huo saa mbili za usiku.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us