MICHEZO
1 dk kusoma
Kenya yatozwa faini ya dola elfu 19 na CAF
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeitoza faini ya dola zaidi ya 19,000 Shirikisho Soka la Kenya (FKF) kufuatia tukio la mechi ya ufunguzi kati ya Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja wa Kasarani Jumapili, Agosti 3, 2025.
Kenya yatozwa faini ya dola elfu 19 na CAF
7 Agosti 2025

Uamuzi wa CAF umeainisha ukiukwaji kadhaa wa usalama katika mashindano ya wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani CHAN 2024.

Kulingana na tarifa rasmi kutoka kwa afisa wa Afisa wa Usalama wa CAF, matukio kadhaa yalikiuka itifaki za usalama, ikiwemo mkanyagano katika moja ya mlango ambao ungesababisha hatari kwa mashabiki uwanjani.

Baadhi ya maafisa, ikiwemo wa CAF na wale wa itifaki hawakuruhusiwa kufika kwenye jukwaa ya watu mashuhuri.

Kenya yatozwa faini ya dola zaidi ya 19,000 na CHAN

Zaidi ya hayo, mlinzi mmoja anadaiwa kumshambulia afisa wa CAF.

Kabla ya mashindano ya CHAN kuanza, serikali na CAF walitangaza hatua kadhaa zilizokuwa na lengo la kuhakikisha usalama na umakini wakati wa michuano hiyo.

Nchini Kenya mechi za CHAN zinachezwa katika viwanja vya Nyayo na Kasarani, huku fainli ikiratiiwa kuchezwa Agosti 30. Kenya ni wenyeji wenza pamoja Tanzania na Uganda katika mechi hizo zinazochezwa kuanzia Agosti 2 hadi Agosti 30.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us