Aliyekuwa spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefariki dunia.
Taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson inasema kuwa kifo cha Job Ndugai, kimetokea Agosti 6, 2025.
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika mstaafu wa Bunge, Job Ndugai kilichotokea leo jijini Dodoma.
Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subiri katika kipindi hiki kigumu,” ilisomeka sehemu ya taarifa ya Dkt. Ackson.
Mwanasiasa huyo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.
Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa ambapo hivi karibuni, alishinda kura za maoni ili aweze kugombea tena nafasi hiyo.