tokea masaa 9
Kwa matokeo hayo, yakizingatiwa pamoja na ya sare ya sifuri kwa sifuri kwa Algeria dhidi ya Niger kwenye kundi C, imewahakikishia Korongo wa Uganda kumaliza kundi hilo wakiwa kileleni kwa mara ya kwanza katika historia yao ya kucheza mashindano ya CHAN, huku Afrika Kusini ikiyaaga michuano hiyo.
Uganda yaweka Historia Kampala
Walihitaji tu sare ili kuingia hatua ya robo fainali, Uganda ilikuwa na kila sababu ya kuamini hilo baada ya goli la Jude Ssemugabi katika dakika 31.
Zilizopendekezwa
Kufikia mapumziko Uganda ilikuwa bado na ushindi huo mwembamba, lakini katika kipindi cha pili ilikuwa ni nipe nikupe na wakati mmoja Afrika Kusini ikafika kuongoza mechi hiyo.
Rogers Torach aliwainua mashabiki wa nyumbani alipoingiza goli katika dakika ya 96, na kupata sare waliyoikuwa wakiihitaji.
CHANZO:TRT Afrika Swahili