AFRIKA
1 dk kusoma
Algeria yalazimisha sare ya 1-1 kwa Guinea. Niger 0-0 Afrika Kusini
Algeria ilisawazisha dakika 88 kupitia Soufiane Bayazid na kulazimisha matokeo ya sare ya 1-1 na Guinea katika mechi ya kundi C ya CHAN 2024 kwenye uwanja wa Mandela nchini Uganda siku ya Ijumaa.
Algeria yalazimisha sare ya 1-1 kwa Guinea. Niger 0-0 Afrika Kusini
CHAN 2024. / CAF
tokea masaa 12

Goli la Ismaël Camara la dakika ya 62 liliwapa Guinea uongozi na wakawa na imani kwa muda mrefu kuwa wanachukua alama zote tatu, lakini Soufiane Bayazid alisawazisha ikiwa imebaki dakika mbili kwa mechi kumalizika na kuendeleza rekodi ya Algeria ya kutofungwa hata mechi moja.

Matokeo haya yamebakisha Guinea ikiwa na alama nne baada ya mechi nne, na matumaini ya kuendelea zaidi ya hatua ya makundi yakiwa na ati ati, huku Algeria ikiwa na alama tano ikiwa bado na nafasi kubwa ya kuingia kwenye robo fainali wakati wakisubiri mechi ya mwisho.

Wenyeji Uganda wanaoongoza kundi hilo la C wana alama sita.

Mechi nyingine kwenye kundi hilo kati ya Niger na Afrika Kusini imemalizika kwa sare ya sifuri kwa sifuri.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us