AFRIKA
3 dk kusoma
Gen Z: Kizazi chenye uwezo ambacho kiko tayari kubadilisha mustakabali
Wamezaliwa katika miaka ya katikati mwa 1990 na mapema miaka ya 2010, Gen Z ni tofauti na vizazi vilivyopita. Ni kizazi cha kwanza kuzaliwa enzi za teknolojia ya kidijitali.
Gen Z: Kizazi chenye uwezo ambacho kiko tayari kubadilisha mustakabali
Vijana barani Afrika ni asilimia 60 ya vijana wote walio chini ya umri wa miaka 25 duniani. / Reuters
tokea masaa 15

Kila mwaka Agosti 12, dunia inaadhimisha siku ya Kimataifa ya Vijana — kusherehekea uwezo, ubunifu, na ari ya vijana wote kila mahali. Kwa Afrika, siku hii ina maana muhimu zaidi. Ikiwa zaidi ya asilimia 60 wako chini ya umri wa miaka 25, bara hilo lina idadi kubwa ya vijana duniani. “kundi hili” halitaki ahadi iliyo mbali; wakati umefika sasa, na namna Afrika inavyowajali itaonesha muelekeo kama mustakabali utakuwa wa maendeleo au fursa iliyopotea.

Gen Z Wamezaliwa katika miaka ya katikati mwa 1990 na mapema ya miaka ya 2010, Gen Z ni tofauti na vizazi vilivyopita. Ni kizazi cha kwanza kuzaliwa enzi za teknolojia ya kidijitali. Wanatumia simu janja, mitandao ya kijamii, na masomo katika majukwaa mbalimbali kwa urahisi, kuwapa nyenzo za kuunganisha, kuunda, na kushindana duniani. Lakini pia wanakabiliwa na changamoto: hakuna ajira, hakuna usawa, na mifumo ya kiuchumi ambayo haiwazingatii.

Benki ya Maendeleo Barani Afrika inakadiria kuwa kila mwaka, vijana milioni 10 hadi 12 wanaingia kwenye soko la ajira, lakini ni milioni 3 pekee wanaopata ajira rasmi. Hii ni changamoto kubwa kwa bara zima. Kama haitashughulikiwa, kuna hatari ya kusababisha hali ya ukosefu wa usalama. Kama litashughulikiwa, linaweza kusaidia kukwamua moja ya fursa muhimu ya kiuchumi katika historia ya sasa.

Tayari, Gen Z wanaonesha dalili za ari yao. Kote barani, kuna ubunifu nchini Nigeria, Kenya na Ghana. Kwa wengi, mitandao ya kijamii siyo tu kwa ajili ya burudani, ni njia mojawapo, ya kupata soko, na jukwaa la kujenga mitandao. Kuongezeka kwa utamaduni wa “kazi za pembeni” kunadhihirisha umuhimu na ubunifu.

Lakini ubunifu pekee hauwezi kubadilisha uchumi. Kwa Afrika kutumia vizuri fursa ya vijana wake, maeneo matatu yanahitaji kuangaliwa kwa makini.

1. Kuwapa vijana mafunzo ya kujiandaa na soko la ajira

Huku Waafrika wengi wakihitimu zaidi kutoka kwenye vyuo kuliko awali, elimu mara nyingi inashindwa kuwa na mtazamo wa kisasa. Serikali na sekta binafsi lazima zifanye kazi pamoja.

2. Vijana wapate mitaji

Kwa wajasiriamali vijana, dhamana za kawaida za benki, kuangalia historia ya kukopa, na kuwa na wadhamini ni vikwazo. Mifumo mbadala ya kupata fedha, inaweza kutatua masuala ya kupata mitaji.

3. Kuweka mifumo ya miundombinu

Kuwahimiza wajasiriamali bila kuwa na miundiombinu sahihi hakusaidii. Kukatwa kwa umeme kila wakati, gharama kubwa za intaneti, na msururu mrefu wa mchakato wa usajili. Serikali zinatakiwa kuona vijana kama washirika muhimu wa kiuchumi.

Siku ya Kimataifa ya Vijana inatoa mtazamo na fursa ya kuangazia vipaumbele hivi. Kote duniani, ujumbe ni ule ule: wakati vijana wanapopata fursa, jamii inafaidika. Hata hivyo barani Afrika, hii siyo tu fursa tu; ni kuhusu kuishi katika dunia yenye ushindani mkubwa. Fursa bila kuchukuwa hatua inasababisha kuharibu nafasi, na hatua bila fursa inasababisha watu kuwa na mfadhaiko.

Kama hiyo haitoshi, bara la Afrika huenda likapoteza wataalamu wake, siyo tu kwa watu kuhama, lakini kupitia “kuhama kidijitali”, ambapo vijana wenye ujuzi wanafanyia kazi mashirika ya nje, wakichangia kidogo kwenye uchumi wa mataifa yao.

Siku ya Kimataifa ya Vijana inatakiwa kuwa zaidi ya sherehe. Inatakiwa kuwa kichocheo cha serikali kufanya mabadiliko, kwa biashara kufunguka zaidi, na kwa jamii kuamini vijana na uongozi wa leo, wala siyo mustakabali.

Historia inaonesha kuwa vijana wakipewa nyenzo, na fursa za kuongoza, wanaweza kubadilisha mitazamo ya mataifa. Katika siku hii ya Kimataifa ya Vijana, swali la msingi ni kama Afrika na dunia itawapa nafasi.

Mwandishi, Shuaib Mahomed, ni Mwanauchumi wa Afrika Kusini ambaye anafanya utafiti wake unaoangazia masuala ya soko la fedha.

 Kanusho: maoni haya ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

 

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us