AFRIKA
2 dk kusoma
Marekani yaiwekea vikwazo kundi la wapiganaji, makampuni ya uchimbaji madini haramu nchini DRC
Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya kundi lenye silaha linaloshirikiana na jeshi la Congo pamoja na kampuni ya uchimbaji madini nchini humo na wafanyabiashara wawili kutoka Hong Kong kwa kutumia silaha na uuzaji wa madini haramu.
Marekani yaiwekea vikwazo kundi la wapiganaji, makampuni ya uchimbaji madini haramu nchini DRC
Vikundi vyenye silaha vinadhibiti maeneo yenye utajiri wa madini./ / Reuters
tokea masaa 16

Hatua hizo ni za hivi punde zaidi zilizochukuliwa na serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani kujaribu kuleta amani mashariki mwa Congo, ambako waasi wa M23 walipiga hatua mapema mwaka huu, na kuzua ghasia ambazo zimesababisha vifo vya maelfu ya watu.

Idara ya Hazina ilisema inaweka vikwazo kwa Umoja wa ‘Coalition des Patriotes Resistants Congolais-Forces de Frappe (PARECO-FF)’, wanamgambo ambao idara hiyo imesema walidhibiti maeneo ya uchimbaji madini katika eneo lenye utajiri wa madini la Rubaya kuanzia 2022 hadi 2024.

Rubaya, ambayo sasa inadhibitiwa na M23, inazalisha asilimia 15 ya madini ya coltan duniani, ambayo husindikwa kuwa metali inayostahimili joto iitwayo tantalum inayohitajika sana na watengenezaji wa simu za mkononi, kompyuta na matumizi mengine katika sekta ya umeme, anga na matibabu.

Vikwazo hivyo vipya, ambavyo vinazuia biashara na makampuni na watu wa Marekani, pia vinalenga kampuni ya uchimbaji madini ya Cooperative des Artisanaux Miniers du Congo (CDMC), ambayo Idara ya Hazina ilisema inauza madini muhimu kutoka maeneo ya udhibiti wa PARECO-FF, na makampuni ya Hong Kong ya East Rise Corporation Limited na Star Dragon Corporation Limited, ambayo ilisema yalinunua madini hayo.

Afisa Mkuu wa serikali ya Marekani, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema Washington ilikuwa inataka kuiwekea vikwazo biashara hiyo haramu "ili kuifanya ivutie zaidi."

Utawala wa Trump unatumai makubaliano ya amani yatavutia mabilioni ya uwekezaji wa nchi za Magharibi katika eneo lenye utajiri wa madini.

Ripoti ya kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa iliyochapishwa mwezi uliopita ilisema jeshi la Congo lilipokea msaada kutoka kwa PARECO-FF mwishoni mwa 2024 na mapema 2025.

Hadi sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa msemaji wa serikali ya Congo na Kampuni ya East Rise. Aidha Star Dragon, CDMC na PARECO-FF pia hazikutoa tamko lolote.

InayohusianaTRT Global - Congo yaongeza marufuku ya kuuza nje madini ya cobalt kwa miezi mitatu
CHANZO:Reuters
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us