13 Agosti 2025
Siku ya Jumatano Sudan Kusini imekanusha taarifa kuwa inafanya mazungumzo na Israel kuwapeleka Wapalestina huko kutoka Gaza, ikisema kuwa “inakanusha vikali” madai ya hivi karibuni ya vyombo vya habari vya Israel kuzungumzia mipango hiyo.
Sudan Kusini “inakanusha vikali taarifa za hivi karibuni za vyombo vya habari zinazodai kuwa Serikali ya Sudan Kusini inafanya mazungumzo na taifa la Israel kuhusu watu wa Palestina kutoka Gaza kupelekwa kuishi Sudan Kusini,” taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje imesema.
Wizara imesema kuwa madai hayo “hayana msingi na hayaashirii msimamo au sera rasmi” ya serikali ya Sudan Kusini.
Imetaka vyombo vya habari “kuwa makini” na kuthibitisha taarifa na vyanzo rasmi kabla ya kusambaza.
CHANZO:AA