AFRIKA
1 dk kusoma
Mali yawakamata wanajeshi, raia wa Ufaransa kwa kuvuruga amani nchini humo
Kati ya waliokamatwa, ni pamoja na raia wa Ufaransa, aliyetambulika kama Yann Vezilier.
Mali yawakamata wanajeshi, raia wa Ufaransa kwa kuvuruga amani nchini humo
Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Assimi Goïta./Picha:Wengine
15 Agosti 2025

Serikali ya kijeshi ya Mali imewakamata majenerali wawili na raia mmoja wa Kifaransa kwa tuhuma za kuvuruga amani nchini humo, chombo cha habari cha Mali kimesema.

Vyanzo mbalimbali viliieleza Reuters kuwa zaidi ya wanajeshi 30 walimetiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusika na uvuragaji amani nchini Mali.

Kati ya waliokamatwa, ni pamoja na raia wa Ufaransa, aliyetambulika kama Yann Vezilier.

Uhusiano wa Ufaransa na makoloni yake yaliyopo katika ukanda wa Sahel baada ya kupinduliwa kwa serikali za kiraia za nchini Mali, Burkina Faso na Niger.

Serikali ya Mali imemtuhumu Vezilier kwa kutumika na Ufaransa kuchochea vurugu nchini Mali.

Kwa upande wake, serikali ya Ufaransa imesema haina taarifa zozote kuhusu kukamatwa kwa Vezilier.

CHANZO:Reuters
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us